Uongozi na wanachama wa asasi ya vijana ya Tanzania Youth Vision Association(TYVA) kwa masikitiko makubwa tunaungana na watu wengine kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya hayati Nelson Mandela, wananchi wa Afrika Kusini, watu wote wa bara la Afrika na dunia yote kwa ujumla kwa msiba huu mkubwa.
Ni wazi dunia nzima ipo kwenye majonzi makubwa kwa kuondokewa na kiongozi shupavu, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini(1994-1999), mtu jasiri asiyeogopa kufa akisimamia ndoto yake ya kupigania uhuru, asiye na uchu wa madaraka, mtu makini, mwerevu, mwenye wingi wa hekima, mtu aliyejali wengine kuliko kujijali mwenyewe, mwenye kuamini katika umoja, mwenye roho ya kusamehe waliomuonea na kumfunga jela kwa miaka ishirini na saba(27), mtetezi wa wanyonge kwa vitendo na sio tu kwa maneno, hayati Nelson Mandela.
Bila shaka alikuwa ni nguzo imara iliyobakia katika kizazi cha viongozi waliopigania uhuru sio tu wa nchi moja moja bali Afrika nzima na dunia yote, akishirikiana na wengineo walioamini kuwa "kiongozi bora ni yule anayetetea maslahi ya wananchi anaowaongoza bila ubaguzi wa aina yoyote, iwe wa rangi, jinsia, ama udini".
Mwisho kabisa, tunatoa wito kwa vijana wenzetu na jamii nzima, tuwe wazalendo na kujiuliza "tutakumbukwa kwa lipi jema?" na watu wa nchi yetu ya Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla kwani alisema hayati Mandela; "sisi pekee tunaweza kuifanya dunia mahali bora pa kuishi".
MUNGU AILAZE ROHO YA HAYATI NELSON MANDELA MAHALI PEMA PEPONI, AMEN!
Wenu katika kujenga taifa,
Naamala Samson,
Makamu Mwenyekiti,
Tanzania Youth Vision Association(TYVA).


.bmp)
Mimi nimezaliwa terehe 18 julai ktk siku kuu ya kuzaliwa Mzee Madiba. Najisikia kupendelewa na Mungu ktk hicho japokuwa miaka tupo tofauti kubwa sana na Mzee Madiba, lakini tarehe na mwezi zinatosha sana , najivunia sana siku yangu ktk tarehe hiyo. RIP Babu yangu Nelson Mandela I'll love You forever. - Mr MHOJA - Sweden
ReplyDelete