Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Sharon L. Cromer ameahidi kuendelea kushirikiana na TFDA katika kuhakikisha afya ya wananchi inalindwa kwa kuisaidia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika kuijengea uwezo kwenye masuala ya udhibiti wa usalama na ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini. 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17/12/2013 katika ziara ya ujumbe wa USAID iliyofanyika Makao Makuu ya TFDA kwa lengo la kujionea ufanisi wa utendaji wa Mamlaka kufuatia misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Shirika hilo la kimaendeleo kwa TFDA kuanzia mwaka 2011 hadi sasa.

USAID imekuwa ikiisaidia TFDA katika kuwajengea uwezo watumishi wake hususan udhamini wa mafunzo kwa wakaguzi wa dawa, mafunzo kwa watumishi kuhusu mifumo bora ya utendaji kazi na utoaji huduma pamoja na manunuzi ya vifaa vya maabara ya Mikrobiolojia kwa lengo la kuendelea kukidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo, alikabidhi tuzo maalum kwa shirika la USAID ikiwa ni alama ya kutambua mchango wa USAID katika mafanikio yaliyofikiwa na Mamlaka kwa kipindi cha miaka 10 (2003-2013). 


Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akikabidhi tozo maalum kwa Mkurugenzi wa USAID Bi. Sharon L. Cromer katika hafla iliyofanyika TFDA makao Makuu.
Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya TFDA na ujumbe wa USAID wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo.



Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akiuonesha ujumbe wa USAID moja ya vitabu rejea vya viwango vinavyotumika katika maabara ya TFDA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...