Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia Mhe. Januari Makamba akiongozana na mkewe Ramona Makamba  wakiwasili ukumbini na kulakiwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchinii Marekani na Mexico Afisa Paul Mwafongo akiwemo Dj Luke wakati walipokuwa wakiingia ukumbini Laurel, Maryland kwenye sherehe ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika Jumamosi Dec 7, 2013 na kuhudhuriwa na umati wa wakazi wa DMV wakiwemo marafiki zao kutoka majimbo ya jirani.
Mhe, January Makamba akiwapa wanaDMV salamu toka Tanzania na kuwaelezea mstakabali mzima wa nchi yetu na kusema miaka 52 kwa binadamu ni mingi lakini kwa nchi bado ni michache aliezezea pia upande wa mawasialiano unavyokuwa kwa kasi na jinsi alivyofarijika kuja kukutana na Watanzania wa DMV na kusema yeye ni muumini mkubwa wa raia pacha kwani anaamini Mtanzania wa Ughaibuni ananafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya nchi yake. Leo Mhe. January Makamba atakutana na WanaDMV Mirage Hall kuanzia saa 11 jioni.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti na Utawala wa Umma Bwn, Georgr Yambesi akielezea mfuko wa pensheni wa PSPF na kuendelea kuelezea faida zake na kwamba sasa mfuko huu umeundwa kutumiwa na hata Watanzania waishio ughaibuni. Leo pia wataongea na Watanzania DMV Mirage Hall Langley Park kuanzia saa 11 kamili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. lovely, mke wake kafanana sana na dada yake mwamy!

    ReplyDelete
  2. Sawa hatukatai uwepo wa Bendera ya Marekani,

    Lakini pia Bendera ya Tanzania ni mojawapo ya bendera zinazo pendaza sana kwa (rangi zake ambazo hakuna umwagaji damu au NYEKUNDU) miongoni mwa Bendera za Mataifa ya Dunia!!!

    Tungefurahi sana mnapo onyesha Bendera ya Marekani angalau na sehemu ya ncha ya Bendera yetu nzuri sana ya Tanzania ionekane!

    ReplyDelete
  3. Sawa hatukatai uwepo wa Bendera ya Marekani,

    Lakini pia Bendera ya Tanzania ni mojawapo ya bendera zinazo pendaza sana kwa (rangi zake ambazo hakuna umwagaji damu au NYEKUNDU) miongoni mwa Bendera za Mataifa ya Dunia!!!

    Tungefurahi sana mnapo onyesha Bendera ya Marekani angalau na sehemu ya ncha ya Bendera yetu nzuri sana ya Tanzania ionekane!

    ReplyDelete
  4. Bendera ya Taifa la TZ iko wapi? Mpiga picha hakugundua kama kuna hitilafu? Sherehe za TZ, Kiongozi wa TZ, bendera ya US?! (I'm assuming bendera ilikuwepo upande mwingine!)

    Ila First Lady mtarajiwa amependeza!!

    ReplyDelete
  5. kwenye hotuba yake Mhe. J. Makamba amesema kwamba hadi 1994 Tanzania ilikuwa na vyanzo vya habari habari viwili tu. Kila habari ilikuwa inatoka either kwenye chama (CCM) au serikali.Tuliaminishwa mambo mengi sana ambayo taifa zima liliamini. Sasa wewe anynoumous hapo juu ulipata wapi hii " Bendera ya Tanzania ni mojawapo ya bendera zinazo pendaza sana kwa (rangi zake ambazo hakuna umwagaji damu au NYEKUNDU)" ??? unanikumbusha zamani tulipokuwa wadogo tunaambiwa Tanzania ni ya pili kwa
    upelelezi dunia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...