Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola barani Afrikaans wakisimama dakika moja ya ukimya ikiwa ni katika kumkumbuka Raid wa kwanza Mzalendo wa Afrika Kusini,Tata Nelson Mandela.Kikao hicho kilifanyika hapo jana katika hoteli ya Bahari Beach.
Spika wa Bunge la Tanzania,Mhe Anne Makinda ambae pia ndio Rais wa Chama hicho barani Afrika akiwakaribisha rasmi wajumbe wa Kamati ya Uongozi.Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2014 unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai na kuhudhuriwa na takriban wabunge 500.
Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...