BAADHI ya vyakula vya asili ya Handeni, vinatarajiwa kuwapo katika Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu 2013 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
 
Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa tayari wametoa nafasi kwa wanaoweza kazi hiyo kwa umakini na usafi wa aina yake ili kuliweka tamasha hilo kwenye mguso wa aina yake.
 
Alisema taratibu zote zimeshafanyika ikiwamo kutembelea vikundi vitakavyotoa burudani, ambapo Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alitumia muda mwingi kuwahamasisha wadau kuhudhuria kwa wingi katika tamasha hilo, kupitia sherehe za Uhuru zilizofanyika wilayani humo Desemba 9 mwaka huu.
 
“Kila kitu kimekamilika, tukiamini kuwa wadau wote watakaohudhuria kwenye tamasha hilo watapata fursa ya kula vyaku7la vya asili, maana pia ni sehemu ya utamaduni wa Handeni.
 
“Sisi tunaamini hili ni tamasha la aina yake ambalo litashangaza watu wengi kutokana na kuandaliwa kwa kiwango cha juu, huku likianzia kwa maandamano katika Ofisi za Halmashauri ya mji Handeni kuanzia saa 2 asubuhi na kuelekea Uwanja wa Azimio,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Mbwana, watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na vyakula wala vinywaji ili kudhibiti suala la afya za watu kwa kupitia tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote, hususan wapenzi wa utamaduni hapa nchini.

Wadhamini katika tamasha hilo ni gazeti la Mwananchi, Clouds Media Group, Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters, Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD), Michuzi Media Group, duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Partnership, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Welewe Walume nyue Wegazi weuwila uno Kukaya Handeni!!!

    1.Izinkande:
    -Vino Imimanda navitendeke viyaho?
    -Maboko mabisi yeyaho?
    -Izinyama za Kwenyika nezitende ziyaho?
    -Makoko na Mayungu yeyaho?
    -Cheluwe na Mpwimbwiji viyaho?
    -M'pombe Nkangala iyaho?
    -M'pombe Lusuwo wiyaho?

    2.Imila nezi ngoma:
    -Makindi yeyaho?
    -Mselego wiyaho?
    -Selo iyaho?
    -Mkwese wiyaho?

    Inatendeka ivyo halanga viyaho nanize Kukaya!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...