Kampuni ya mawasiliano ya simu, Vodacom Tanzania leo imeendesha mafunzo kwa watumishi wa kituo cha mafuta cha OilCom kilichopo kwenye makutano ya barabara ya Libya na Morogoro kuhusu huduma ya kulipia kwa njia ya M-pesa.
M-pesa na OilCom walizindua huduma inayowawezesha wateja wao kulipia kwa njia ya M-pesa wanapopata huduma kwenye vituo vya OilCom vya TMJ Msasani, Kipawa na Libya.
“Tunawapatia mafunzo wateja na watumishi kwenye vituo hivi ili kila mmoja aweze kunufuika na kile tunachowapatia kupitia M-pesa.
"Tunafurahi kuona huduma hii imepokelewa vizuri na inatumika bila ya shida yoyote.”Alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Salum Mwalim.
“Lengo letu kuu ni kujua mandeleo ya huduma yetu ni jinsi gani inatumika hapa, tumekuja kupata maoni ya wauzaji pamoja na wateja wao pia kuwaelekeza pale wanapokwama. Hatutaki yale tuliyokubaliana siku ya ubia yaishie kwenye vyombo vya habari, tunataka kupata maoni ya wateja wetu moja kwa moja ili tuwasaidie.” Alisema Salum
Salum
Aliongeze kuwa kutembelea kunawasaidia sana wateja wao na hata kuwaondelea wasiwasi juu ya huduma ya M-Pesa na kwamba watafanya hivyo kwenye vituo vyote vya OilCom ambapo huduma ya M-pesa inapatikana.
Akizungumza kituoni hapo Meneja wa IT wa kampuni ya OiCom Abubakar Mohamed amesema huduma hiyo iliyozinduliwa wiki tatu zilizopita yayari imeshakubalika kwa wateja na kwamba wameifurahia kw akuwa inawaondolea usumbufu wateja wao.
"Tumefurahi sana na inakwenda vizuri. Mipango inaendelea kuahkikisha vituo vyote vya OilCom vya jijini Dar es salaam vinawezeshwa kufanya malipo kwa njia ya M-pesa.”Alisema
Amesema wateja wateja wa OilCom hawana sababu yoyote ya kutoitumia njia ya M-pesa kufanya malipo kwenye vituo ambavyo tayari vimeshawezeshwa na kwamba kampuni yake imejiapnga kisawasawa kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake.
Esmail Abdulrahaman ni mmoja wa wateja waliofika kujaza mafuta kituoni hapo, kwa upande wake yeye amesema “Huduma hii ini nzuri na inaleta urahisi sana ni vema tunajua uwepo wake na hakuna shak inatushaiwhsi kuitumia ili kuondoa usmbufu na utegemezi kwenye njia moja tu ya malipo ya fedha taslimu.”
Kwa upande wake Mahmud Mohammed lisema kuwa yeye ni mteja mzuri sana wa mafuta ya kituo cha Oilcom na kudhihirisha kuwa huduma hii imemletea faraja kubwa sana kwani kwa sasa hatokuwa akibeba fedha nyingi badala yake kuziweka kwenye akaunti yake ya M-Pesa na kufanya mizunguko yake akiwa na uhakika kwa kuweka mafuta kwenye gari lake.
Hivi karibuni kampuni ya Vodacom Tanzania na Oilcom ziliingia ubia ambapo wateja wa pande zote mbili wamewezeshwa kulipia mafuta kwa kupitia huduma ya M-Pesa popote kwenye vituo vya kampuni hiyo ya mafuta.
Kwa kuanza, uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam na kituo cha mafuta cha TMJ Msasani kikiwa cha kwanza kuunganishwa na huduma hiyo huku vingine viwili vimefatia kisha huduma hiyo kusambaa nchi nzima palipo na huduma ya M-Pesa na vituo vya mafuta vya Oilcom.
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimjulisha Mahmud Mohamed aliyefika
kujaza mafuta kwenye kituo cha OilCom kilichopo kwenye makutano ya barabara ya
Libya na Morogoro jijini Dra es salaam kuhusu kuwepo kwa huduma ya malipo kwa
njia ya M-pesa kituoni hapo. Kushoto ni Meneja wa IT wa kampuni hiyo ya mafuta
Abubaka Mohammed. Huduma ya malipo kwa M-pesa inapatikana pia kwenye vituo vya
OilCom vya TMJ Msasani na Kipawa.
Meneja
wa IT wa Kampuni ya OilCom Abubakar Mohamed akiongea na waandishi wa habari
wakati wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa kituo cha OilCom kilichopo kwenye
makutano ya Barabara ya Libya na Morogoro.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Salum Mwalim na kulia ni Meneja Msaidizi wa kituo hicho Hussein Ahmed.
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiwapa mafunzo wahudumu wa kituo cha
mafuta cha OilCom kilichpo katika makutano ya barabara ya Libya na Morogoro
jijini Dar es salaam juu ya namna ya wateja wanaojaza mafuta kituoni hapo wanavyoweza
kulipia kwa njia ya M-pesa. Huduma ya malipo kwa M-pesa inapatikana pia kwenye
vituo vya OilCom vya TMJ Msasani na Kipawa.
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akionge na Mteja wa OilCom Esmail
Abdulrahaman kuhusu kuzinduliwa kwa huduma ya malipo kwa M-pesa kwenye vituo
vya OilCom Msasani TSJ, Makutano ya barabara ya Libya na Morogoro na Kipawa
jijini Dar es salaam. Kulia ni mtumishi wa OilCom Ala Mohammed.
Katika vituo vya mafuta ki-usalama simu hazitakiwi. Sasa tunakubali kulipia mafuta kituoni na simu. Likitokea janga ndio tuweke sharia? Naona hatuko makini
ReplyDeleteNdugu yangu wa kwanza, unaweza kutoa sababu kwanini unasema simu haziruhusiwi kwenye vituo vya mafuta? Simu zinatumia electromagnetic waves ambazo hazina uhusiano wowote na maswala unayoyasema. Marekani ruksa kutumia sim hata kwenye ndege.
ReplyDeleteAcha kusemasema mambo ambayo huwezi kuyatolea ufafanuzi ndugu yangu