MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar jana wakati alipokuwa akielezea maandalizi ya lala salama ya tamasha hilo,linalotarajiwa kufanyika siku ya sikukuu ya Krisimasi,kwenye Uwanja wa Taifa.

Tamasha hilo litakalojumisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za kiroho wa hapa nyumbani sambamba na kutoka nje ya nchi ikiwemo nchini Afrika Kusini na Rwanda.Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu na Liliani Kabaganza kutoka nchini Ruanda wanatarajiwa kuwasili jijini Dar leo tayari kwa ushiri wa tamasha hilo linalowakutanisha watazamaji lukuki.
MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akiwataja baadhi ya Waimbaji watakatumbuiza kwenye tamasha hilo la Krisimas,kuwa ni Rose Muhando,Solomon Mukubwa,Upendo Nkone,Upendo Kilahiro,Anastazia Mukabwa,John Lissu,Boni Mwaitege,Ephrahim Sekeleti,Glorious Warship Team,The Voice Acapella,New Life Band na wengineo kibao.Msama alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekwishakamilika na kinachosubiriwa mashambulizi tu yatakayoanzia jijini Dar,Morogoro,Tanga,Arusha na kumalizia mkoani Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...