MKUU wa wilaya ya Mtwara,Willman Ndile amewahimiza wakazi wa Manspaa ya Mtwara Mikindani kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni ya kufanya usafi wa mazingira ya mji aliyoianzisha ili kuuweka mji uo katika hali ya usafi.
Ndile aliyasema hayo alipokuwa akiongea mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi jana katika eneo la Bima mjini hapa ambapo alisema, ni jambo jema wananchi wanapojitokeza kushiriki katika shughuli za kijamii kuoneshwa namna ambavyo serikali inajali mchango wao licha ya kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.
Alisema katika siku ya kwanza ya kampeni hiyo wananchi wengi wamejitokeza hali inayomtia hamasa zaidi kuendeleza kampeni hiyo na sasa itakuwa ikifanyika kila siku ya mwisho wa wiki na kuwataka viongozi wa mitaa na kata kuweka mikakati na mipango mizuriya kutekeleza zoezi hilo katika maeneo yao.
Hatua hiyo ya Mkuu huyo wa wilaya kuanzisha kampeni hiyo inatokana na kukithiri wa uchafu kwenye maeneo ya Manspaa ya Mtwara Mikindani huku mamlaka husika zikitupiana lawama kati yao na wananchi na taasisi mbalimbali kuwa ndio wenye jukumu la kufanya usafi hali inayofanya kuwapo kwa vichaka katikati ya mjini na marundo makubwa ya takataka katika makazi ya watu.
Katika kampeni hizo watu mbalimbali walijitokeza wakiwemo wakazi wa manspaa, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, watendaji wa serikali na waandishi wa habari ambapo walishiriki kufanya usafi katika eneo ya kandokando ya barabara kuu itokayo Mnarani hadi bodi ya korosho.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara,Willman Ndile (Aliyeshika kidumu) akishiriki katika kampeni ya kufanya usafi wa mji ambapo viongozi wa siasa, watendaji wa serikali na wananchi wengine walishiriki kampeni hiyo inayofanyika kila mwisho wa wiki.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile, akikusanya takataka tayari kwa kuzichoma moto, kama anavyoonekana hapa eneo la CRDB mjini Mtwara.
Katibu tawala wa wilaya ya Mtwara mkoani hapa, Nuru Ringo, akishiriki katika kampeni ya usafi wa mji iliyoanzishwa na mkuu wa wilaya hiyo, Willman Ndile, hapa anaonekana akizoa matawi ya miti iliyopanguliwa pembezoni mwa barabara eneo la Bima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...