Jumuiya ya Watanzania Jijini New York na Vitongoaji vyake jana Jumamosi imesherehekea miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, katika Hafla iliyojaa nderemo, shamrashamra zikiambatana na muziki, chakula, vinywaji na maonyesho ya nguo zilizokuwa na maudhui ya utamaduni na desturi ya mtanzania. Sherehe hizo zilitanguliwa na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Timu ya New York na Timu ya ....... ambako timu ya New York iliibuka kidedea.

Mgeni Rasmi katika sherehe hizo zilifana kianina yake alikuwa ni Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozit Tuvako Manongi ambaye alifuatana na Naibu wake Balozi Ramadhan Mwinyi na tukaungwa mkono na Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa . Watanzania hawa alisimama kwa sekunde Moja, kumukumbuka na kumwombea Marehemu Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini Huru, Mzee wetu Nelson Mandera.

katika Salamu zake fupi alizozitoa kwa watanzania hao wa Jiji la New York na Vitongoji vyake, pamoja na kuishukuru Jumuia hiyo ya Watanzania kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo, Balozi Tuvako Manongi amewaasa watanzania hao kuendeleza na kujenga misingi ya utaifa, uzalengo, kupendana na kuheshimiana.

Akasema kila mtanzania anayohaki ya kuwa mfuasi wa chama chochote kile cha siasa, lakini jambo kubwa na la msingi linalowaunganisha watanzania popote pale walipo si itiakadi za vyama bali ni utanzania wao ambao umejengekea katika misingi ya utaifa, uzalendo, kuheshimiana, kupendana , kusaidiana ikiwa ni pamoja na kuitetea nchi yao.

Kwa upande wao, Jumuiya hiyo ya Watanzania katika Salamu zao kwa Serikali kupitia Balozi Manongi, wameomba suala la uraia wa nchi mbili lipewe umuhimu wa pekee katika mwenendo mzima wa mchakato wa Katiba mpya unaoendelea.
 Joy na Maurus wakiwaongoza watanzania kuimba wimbo wa Taifa.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akizungumza  machache.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongereni wana NY. Tukarubusheni na sisi wa majimbo mengine

    ReplyDelete
  2. Safi sana kwa kulipa jina Tanganyika haki yake.

    Wengine wanatuchanganya tu; mara uhuru wa Tanzania,mara uhuru wa Tanzania bara...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...