Watu wote mnakaribishwa siku hii ya uhuru kutakuwa na vyakula, vinywaji music na mambo mengi ya kuchangamsha. Unachotakiwa ni kulipa 30$ tu mlangoni njoo tusherekehe siku yetu watanzania kufika kwenu ndiyo mafanikio ya sherehe hii. Sherehe zitaanza saa 11 na nusu jioni njoo mapema uwahi meza yako, usije kula chakula na kunywa ukiwa umesimama chakula kikakimbilia miguuni na ukashindwa kucheza music. Ma DJ wetu bora watatuchezesha mwendo wa ndombolo na rusha roho hadi kukuche, (Dress to Impress) Wote mnakaribishwa. Ukitaka kufika kwa kutumia train chukua N, Q kwenda Queens hadi 36Th Street, Na tembea mtaa mmoja hadi 37Th St kunja kulia jengo litakuwa mkono wako wa kushoto.
Ticket zimeanza kuunzwa mbele ya desk la Tanzania Mission New York. Na pia unaweza kupa ticket hizo kupitia kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo ya uhuru, kwa kupiga # hizi za simu, #347 663 0781, #917 557 3195, na #347 475 4313 pata ticket yako sasa.
Address
Address
Claudio's Cafe II,
32-23 37th Avenue.
Siku hiyo kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya New York na New England (Umoja) Springfield Boston hapa New York wachezaji kuwahi mapema mchezo utaanza saa 8 mchana. Team ya New York baada ya kujifua sana huu ni mchezo wao wa kwanza, wachezaji wamejipanga vizuri ili kuwafundisha mpira team ya Springfield. Baada ya majigambo ya pande mbili kila mmoja akisema ni zaidi ya mwenzie sasa siku ya uhuru jumamosi ya tarehe 7 mzizi wa fitina unakatwa, ukisikia PAHHHHHHHHH labda itokee tuuuuuu!!! |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...