Mwakilishi kutoks IOGT-NTO, Gunnar Lundstom akiwasilisha mada katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
 Mganga wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Iringa na Mratibu wa madhara ya pombe afya mkoa,Dk. Ally Ngala akizungumza katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
 
========  ======  ======== 

WATU MILIONI 2 HUFARIKI DUNIA KWA POMBE

Na Denis Mlowe na Pauline Kuye, Iringa

UTAFITI uliofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya imebainika kuwa watu milioni mbili hufariki kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya pombe.

Hayo yameelezwa na Mganga wa Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Iringa Dk. Ally Ngala wakati akizungumza  katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini hapa.

Dk.Ngala alisema asilimia 4 ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa husababishwa na matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi na kusababisha madhara mengi zaidi kwa watumiaji wa pombe ikiwemo mama wajawazito kuzaa mtoto kabla ya miezi tisa (njiti).

Alisema utafiti huo ulifanywa Februari na Octoba 2012 ulibainisha asilimia 26.8 mpaka 31.9 sawa na watu milioni 15 nchini Tanzania wanatumia pombe, na kati ya hao asilimia 27.4 ya wanaume wanywaji wa pombe ni  walevi kupindukia na  huku  wanawake ikiwa ni asilimia 13.4.

Aidha Ngala alisema  hunywaji wa pombe una hasara nyingi na  kubwa sana kuliko faida zake na alibainisha kuwa hasara mbaya za pombe kwa mtumiaji  ni upande wa kiafya.

“Pombe ina hasara kubwa sana kwa binadamu kiuchumi kwa kusababisha umaskini kifamilia lakini kwa upande wa afya ndio zaidi hii inatokana na kuwa na mchango mkubwa katika kuleta magonjwa, ingawa sio kila ugonjwa husababishwa na pombe pekee” alisema Dk. Ngala

Ngala alisema madhara mengine ya unywaji wa pombe kupita kiasi ni kusababisha  ugonjwa wa Ini kwa  kufa kwa seli za ini hivyo baadaye ini linapoteza uwezo kabisa kwa kushindwa kufanya kazi hivyo kusababisha vifo vingi kwa ugonjwa huo.

Alibainisha pombe husababisha kansa za tumbo na kansa ya kongosho na mtumiaji wa pombe kwa kiasi kikubwa watoto huzaliwa katika hali ya utegemezi wa pombe(Fotal alcoholic syndrome) ambayo huweza kumpotezea maisha mtoto ndani ya mwezi wa kwanza au utaahira wa kudumu(matatizo ya akili).

Alisema  pombe huathiri kiasi kikubwa watumiaji  mfumo mzima wa uzazi na hata kupelekea mtumiaji kupoteza uwezo wa kuzaa kabisa, na huanzia  kupoteza siku za hedhi kwa mwanamke.

Aliongeza madhara mengine ya unywaji wa pombe kupita kiasi ni chanzo kikubwa cha ajali za barabarani na kusababisha hasara kubwa kwa taifa kwa ujumla. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. What? fotal????, it should have been foetal

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...