Klabu ya Yanga imeanza kunufaika na haki za matangazo ya Televisheni baada ya kutangaza kusaini mkataba na kampuni ya SGM ya nchini Kenya kwa ajili ya kuonyesha mechi yao ya raundi ya kwanza dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu (pichani) aliwambia waandishi wa habari jana kuwa mkataba waliongia ni wa mechi moja tu dhidi ya Al Ahly itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa na tayari Yanga wameweka kibindoni dola 55,000 ambazo ni sawa na Sh90 milioni kwa mchezo huo.
" SGM imejipa inaamini Yanga itavuka raundi ya awali dhidi ya Komorozine ya Comoro na kwenda kukutana na mabingwa Afrika, Ahly katika raundi ya kwanza."alisema Njovu
Alisema haki za matangazo ya Televisheni za mechi ya ugenini wamepewa kampuni ya MGB ya Cairo, ambayo itarusha matangazo hayo kwa nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati pekee.
Katibu huyo mpya wa Yanga ambaye amechukua mikoba ya Lawrance Mwalusako alisema televisheni za Tanzania ambazo zitataka kuonyesha mechi hiyo, zitatakiwa kuwasiliana na kampuni ya SGM kupata haki hiyo.
Kuhusu mchezo wa marudiano utakaofanyika Misri, Njovu alisema kuwa wao watakuwa ugenini, watawasiliana na wenyeji wao ili uwezwe kuonyeshwa kwa Tanzania pekee.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa SGM Francis Gaitho alisema wana matumaini makubwa Yanga itaitoa timu ya Comoro na ndiyo maana wamechukua hatua hiyo.
Yanga itaanza na Komorozine ya Comoro katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wakiitoa watacheza na Ahly katika raundi ya Kwanza.
Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Febaruai 7, 8 na 9, wakati marudiano yatakuwa kati ya Februari 14, 15 na 16 February 2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...