Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.


Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.

Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.


kikosi cha blog ya Mbeya yetu  Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni  chupa na dishi  hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

Katibu msaidizi wa hospitali ya  Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida Mwanamke mmoja, Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.'

Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi. 

Kwa mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi aliyemfanyia huduma mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi huyo ni miongoni mwa wazazi 9 waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku yeye akivunja rekodi kwa kujifungua watoto wanne kwa njia ya kawaida. 

Muuguzi huyo alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa mtoto  wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilogramu 1.6,1.5,1.5  na  2.0 ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo wapo katika Chumba cha Joto hadi sasa. 

Aidha kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo. 
Alisema kwa hivi sasa watoto wananyonya vizuri amb  po maziwa yakipungua kwa mama itahitajika msaada wa maziwa ya Kopo aina ya Laktojeni ili watoto waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na afya zao kuimarika.

Kwa upande wake Mzazi wa watoto hao Aida Nakawala alisema hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao na kuongeza kuwa mume wake ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda hivyo anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.

Alisema huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka saba, anayefuata ana miaka miwili na miezi tisa huku mwingine akiwa amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla ya uzao huu unaofanya kuwa na watoto Sita.

Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao alisema Mama yake mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye .

Hata hivyo kutokana na kuguswa kwa  mahitaji ya binti huyo na wanawe kikosi cha blog ya Mbeya yetu ambacho kilifika kumju ulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kadogo hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. The mdudu,,anasema hii ni dalili tosha kabisa toka kwa mwenyezi mungu yakua nchi yetu ni ya AMAANI na NEEMA tele ndio maana ametuletea hawa watoto kwa mkupuo mmoja tena ndani ya mwaka mpya ili waishuhudie katiba yao mpya ya TANGANYIKA,,ombi langu kwa watanzania wenzangu hasa hasa WABUNGE,,MAWAZIRI,,WAKUU WA MIKOA,,WAFANYA BIASHARA WAKUBWA,akina AZAM TEAM,MO wa Singida,MENGI,MANJI,KUSAGA wa Mawingu radio,na wengine kibao tuna hitaji kuona Michango yenu ya kuinasua hii FAMILY ili nao waishi kama nyie nakufaidi matunda ya nchi yao wala si lazima kila mtanzania atoe alicho nacho hao tu niliosema tosha kabisa kuinasua hii family yetu.SUGU uwe wa kwanza

    ReplyDelete
  2. Ukitaka kumsaidia huyu dada muhusika ni nani?

    ReplyDelete
  3. Ni kweli mama wanne huyu anahitaji msaada watoto wanne ni kazi kweli kweli. haraka haraka kutoka experience mahitaji ni kama yafuatavyo:
    1. Kunyonyesha itakuwa kazi hivyo atahitaji formula kwa wingi
    2. atahitaji wasichana wawili (nannies) wa kumsaidia kubembeleza watoto
    3. atahitaji daipas maana kufua nepi nyingi hivi ni kibarua
    4. chakula kwa wingi kwa mama mzazi
    5. chumba cha watoto na vyandarua - kama hajaandaa
    6. Msaada wa pesa za matumizi kwa angalau mwaka mmoja maana hatakuwa na uwezo wa kufanya shughuli za kujipatia kipato
    7. Msaada wa matibabu kwa hospitali iliyo karibu nae (mambo ya chanjo na emergency )
    8. Matibabu kufuatilia hali ya mama, kuna kupoteza damu nyingi na mambo mengineo baada ya uzazi
    9. nguo za watoto za kutosha ili afue anagalau mara moja kwa siku
    Jamani kutoa ni moyo - hebu tuanze mwaka mpya kwa kumsaidia mama huyu

    ReplyDelete
  4. tunaomba namba ya simu kwa mawasiliano ili huyu mama aweze kusaidiwa na wadau

    ReplyDelete
  5. Kweli nampa pole na hongera huyu dada. Nina mapacha na kazi yake si lelemama sasa wanne kweli atahitaji kila kinachowezekana kupatikana. Watu wasianze kufungua midomo hapa mwenye mzigo yupo wapi.. manake hawakuomba watoto wanne wao walijua atakuja mmoja tuu. Hivyo kama alivyosema mdau hapo juu ni kweli tupu. Michuzi tunaomba tujue watoto ni wajinsia gani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...