Si mara nyingi mtuunaweza kuapata bahati ya kukutana na kula taswirazzzz ya aina hii. Lakini Ankal amepata bahati hiyo ya kuonana ana kwa ana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhan Dau (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango kabambe wa kugawa kompyuta aina ya Tablet kwa wanafunzi wa sekondari uliofanyika Jumatatu katika shule ya sekondari ya wasichana ya WAMA Nakayama kijiini Nyamisati Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani.
Dkt Dau ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa shule hiyo wakati Bw. Erio aliiwakilisha PPF kama mgeni mwalikwa, ambapo PPF ni moja ya wafadhili wa shule hiyo ambayo inasomesha bure mamia ya wasichana walio katika mazingira magumu ya kimaisha ikiwa ni pamoja na yatima na wanaotoka katika koo masikini zisizoweza kosomesha watoto wao.
Majabali wawili hawa ni moja kati ya watendaji wanaoongoza kwa ufanisi mifuko ya pensheni nchini. Zaidi kuhusu siku hii BOFYA HAPA
Kweli 'bahati ya mtende, kuotea jangwani' nadhani sio kwa ankal peke yake kukutana uso kwa macho na hao jamaa, bali pia hata kwa WAMA Nakayama Girl's Secondary School nao wamebahatika kupata hiyo opportunity ya kuingia kidigitali na kuweza kupatiwa hizo Tablets ambazo already pre-loaded with educational materials. Ni mpango na mwanzo mzuri, pongezi za dhati na za pekee kwa wote waliohusika kuuwezesha na hatimae kuufanikisha kivitendo mpango huu.
ReplyDeleteDuhhh Mjomba ama kweli Mwaka umeunza vyema!
ReplyDeleteSio rahisi, Mtu kupata bahati ya kukutana na Wakubwa wawili (2) tena walio waungwana sana Wakubwa wa Mifuko ya Mapesa?
Kweli Watanzania akili zetu ni matope, badala ya kununua MADAWATI watoto wasikae chini tunanunua TABLET ili tujionyeshe mbele ya dunia kwa faida ya mama wakwanza. Hungu ndiye mjuzi wa kila jambo
ReplyDeleteMkonooozz uliahirisha au iliukuwaje ankal!!!!! Nice picture
ReplyDeleteWewe mchangiaji amae akili yako ni matope una hakika kama hiyo shule haina madawati au unatapika tu. Kama wao tayari wana madawati wasipewe huduma nyingine mpaka shule ya kijijini kwako ambako na wewe hutaki kuchangia ukiisubiri serikali ikuletee ndo wao wasonge mbele?
ReplyDelete