Bendi ya Mlimani Park Orchestra almaarufu kama Sikinde inategemea kuburudisha wapenzi wa muziki wa dansi kutoka Dar es Salaam kesho Ijumaa (31 Januari 2014) katika ukumbi wa Meeda Sinza wilayani Kinondoni.
Akizungumza kwa niaba ya bendi ya Sikinde, Katibu wa bendi hiyo Hamis Mirambo amesema “baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya shoo yeyote katika wilaya ya Kinondoni ,bendi ya Sikinde sasa ipo tayari kuwakosha moyo za wapenzi wa muziki wa dansi katika wilaya hiyo pamoja na watu wa wilaya za jirani.”
“Tunapenda kuwaalika wapenzi wote wa muziki wa dansi wasikose kuhudhuria shoo yetu ambayo itaanza ukumbini Meeda kuanzia saa mbili usiku,” alisema Mirambo.
Aliongeza, “Karibuni mpate kuburudika na nyimbo za zamani na mpya kutoka bendi hii kongwe hapa nchini. Mpate kusikia kutoka kwa msanii Bichuka na wengine wengi…karibuni sana!”
Kwa hivi sasa bendi hiyo ya Mlimani Park Orchestra inamalizia kukamilisha albamu yao mpya iitawayo “Jinamizi la talaka” ambayo inabeba nyimbo kama Kibogoyo, Deni ntalipa, Ng’ombe haelemewi nunduwe, Kukatika kwa dole gumba, Tabasamu na Mkwezi.
Safi sana, Tunafurahi sana sana Wazee wa Nginde , Karibuni sana Meeda mje mtupe Burudani, ila wengine kama sisi hata mkipiga wapi tupo pamoja
ReplyDeleteDr Ntamamiro Zephania Mzee wa Nginde