Na Edwin Moshi,Makete
Jeshi la polisi wilayani Makete  mkoani Njombe linamshikilia  Fransis Pilla (36) mkazi wa kijiji cha Iwawa na kata ya Iwawa  wilayani hapa kwa makosa  mawili ya  utekaji nyara na  ubakaji  kwa binti mwenye umri wa miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.
Akiongea na vyombo vya habari wilayani hapa afisa upelelezi wa jeshi la polisi wilaya ya Makete Bw Gozbert Komba  amesema kuwa siku ya tarehe 15 mwezi huu walipokea taarifa  kutoka kwa msamaria mwema ambaye pia ni mwajiri wake bw. Erick Mbilinyi (34) ya      mtendewa kutekwa na kufungiwa ndani ya nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake maarufu kwa jina la pagale ambapo walifika katika jumba hilo  na kumkuta akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni.
Amesema kuwa  mara baada ya kumkuta mtendewa huyo akiwa ametekwa walimhoji na yeye kukiri  kuwa amebakwa na  hajaoga tangu afanyiwe ukatili huo na hivyo kurahisishia  kupatikana kwa vipimo kutoka kwa madaktari kuwa ni kweli binti huyo amebakwa na kuongeza kuwa walikuwa wana mahusiano ya kimapenzi.
Katika hatua nyingine mrakibu huyo amebainisha kuwa  mtendewa huyo alisema kuwa alitekwa nyara kwa siku tatu,   na hajala chakula kwa siku zote hizo ambapo alitekwa nyara tangu tarehe 3  mwezi Januari mwaka huu  majira ya saa saba mchana  mpaka tarehe 5 mwezi huu majira ya saa saba na nusu mchana. 
Amesema polisi wanatarajia kumfikisha mahakamani siku chache zijazo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...