CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha na Uchumi na Mbunge wa Kalenga, Dkt. William Mgimwa ambaye amefariki akiwa kwenye matibabu Afrika Kusini.
Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kinatuma salaam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na msaidizi wake wa karibu na mtumishi mwenzake serikalini.
Chama kinatoa salaam za dhati kwa familia ya marehemu Mgimwa kwa kuondokewa na baba na mpendwa wao, katika wakati ambao tunaamini walikuwa bado wakimhitaji sana kama moja ya nguzo za familia.
CHADEMA pia inatuma salaam za pole kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na msiba huo wa kuondokewa na mmoja wa wanachama na wabunge wake.
Mwenyezi Mungu awapatie moyo wa subira wakati huu wa majonzi mazito ya kuondokewa na mpendwa wao, Dkt. Mgimwa.
Kutoka:Kurugenzi ya Habari-Chadema

The mdudu,,anasema huo ndio ukomavu wa kisiasa na uzalendo uliotukuka coz ccm siowote mizigo au serikalini kwa mtazamo wangu wa hari ya juu kabisa Rais wetu ni mzalendo kwa taifa na watu wake woote ila watu wake aliowaamini na kuwateua kuwa Mawaziri au wasaidizi wake ndio wanaomuangusha na kulipeleka taifa siko,,angalizo kwa rais atakae mlisi rais wetu mpendwa kikwete, azingatie huu ujumbe toka kwangu,,MAAMUZI MAGUMU IWE LAZIMA kwa mtu mzigo au kiongozi mzigo,,TANZANIA KWANZA,,IWE mwiko kiongozi wowote au mtanzania yoyote kupelekwa nnje ya nchi yetu kwa matibabu hapa ninamaana tujenge mahospitali ya magonjwa yote hapa nchini tunataka mataifa mengine ndio walete wagonjwa wao sio sisi tena,,MRA RUSHWA na Mtoaji kama walikua mjini wapelekwe vijijini huku wakiwa wamefilisiwa mali zao,na huko vijijini wawe chini ya uangalizi wa mjumbe wa nyumba kumi,ni hayo tu kwaleo,,n RIP DR MGIMWA rill we gonna miss u
ReplyDeleteAsante mdudu kakakuona, una mawazo mazuri sana tangu nimekufuatilia. Lakini hata nyie mlio huko nje jaribuni kufanya kitu nchini jamani. Msijibweteke tu huko. Waconvinceni wazungu hao watusaidie na sisi tuwe na hospitali nzuri nyumbani ikiwa kama mchango wenu. Au unaonaje? ni mawazo yangu. Mdau bongo
ReplyDeleteNdugu yangu usikonde na mm tunaingejea kwa hamu kubwa hiyo katiba ya Tanganyika kwa michango yetu ya mawazo tanganyika yetu itapaa kwa kasi ya ajabu,,asante kwa kumfatilia The mdudu ipo siku tutaonana mdau
ReplyDelete