Mkurugenzi
Mkuu wa COSTECH Dr Hassan Mshinda akifafanua mbele ya wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Miundo mbinu waliotembelea COSTECH mapema leo jinsi COSTECH
inavyojitahidi kusomesha watafiti ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa
Watafiti nchini .Kwa kipindi cha mwaka
2010 hadi 2013 COSTECH imesomesha
jumla ya Watafiti 386 kutoka Taasisi za Utafiti na Vyuo Vikuu kwa shahada ya
Uzamili na uzamivu.Mwaka 2013/2014 Jumla ya Watafiti 131 wamekwishafadhiliwa na
COSTECH wakiwemo 85 wa shahada ya uzamili na 46 wa shahada ya uzamivu.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Dr Patrick Makungu akitoa
ufafanuzi kwa Kamati ya Bunge juu ya namna COSTECH iliyo chini ya wizara
yake inavyokutana na changamoto ya
kushuka kwa fedha za kugharamia utafiti kila mwaka.
Mjumbe wa
Kamati ya Bunge ya Miundo mbinu Mh Zarina Shamte Madabida akipata ufafanuzi juu
ya kazi zinazofanywa na Atamizi ya Dtbi iliyopo chini ya COSTECH.
Mkurugenzi
wa Ubunifu,Ujasiriamali na Ushindani wa COSTECH Dr Dugushilu Mafunda(katikati)
akitoa ufafanuzi kwa Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundo Mbinu Mh Rebecca Michael
Mgodo(wa kwanza kulia) jinsi Kurugenzi
yake inavyofanya kazi za kuendeleza ubunifu,ujasiriamali na Ushindani nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...