Shirika la majisafi na majitaka Dar es salaam(DAWASCO) imesema inawadai wateja sugu Tsh 40 bilioni huku ikiwataka kulipa madeni ili kunusuru utendaji wa shirika.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya DAWASCO kukatiwa huduma ya umeme na TANESCO kutokana na deni la sh 6.3. Hayo yamesemwa na afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO, Eng Jackson Midala alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki. Alisema mamlaka hiyo imeshindwa kulipa kulipa deni hilo kwa wakati kutokana na kuwadai wateja wake zikiwemo taasisi za serikali zaidi ya bilion 40.alisema deni hilo linahusisha baadhi ya taasisi za serikali na watu binafsi.

“kuna hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Jeshi la Wananchi wa Wanzania (JWTZ), Polisi na wengine wengi.hatuwakatii huduma kwa sababu ya madeni ila tunasisitiza kulipa madeni hayo ili na sisi tuweze kulipa mzigo wa madeni mengine ya umeme” alisema Midala Alisema “hivi karibuni mtambo wa ruvu juu uliharibika na mafundi wetu walifanikiwa kuutengeneza, lakini siku ya jumamosi umeme wa TANESCO ulikatwa kwasababu ya deni, jambo lililosababisha Maji kukatika tena kwenye sehemu nyingi za jiji la Dar es salaam” Pia midala alisema kuhusu hatua zinazoendelea kuwashughulikia wateja wanaoiba Maji kwa njia za kuharibu mita kwamba mpaka sasa wamewakamata watu 284 na kuwafikisha mahakamani.

Alisema miongoni mwa watu hao, watatu walihukumiwa adhabu ya kifungo, watatu kesi zilifutwa kwa kukosa ushahidi na wengine kesi zao zinaendelea.

Aliwataka wateja kulipa Ankara zao kwa muda, lengo likiwa kuwezesha mamlaka hiyo kujiendesha na kuendelea kuwapa huduma na pia kutoa taarifa za wizi wa Maji na uharibifu wa miundo mbinu kupitia simu yake ya Mkononi 0779-090900.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Eng Jackson Midala akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matukio mbalimbali ya shirika lake kwa mwaka 2013 na mategemeo ya uboreshaji huduma kwa mwaka 2014.Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Dawasco,Everlasting Lyaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hawa DAWASCO wanashangaza. Wao hawaoni tabu kuitisha waandishi wa habari na kufanya mahijiano. Wanajua kuwa na wao kwa upande mwingine ni kero kwa wananchi kwa huduma zao mbovu? Waanzie na Yasini wa DAWASCO BOKO. Apigwe msaaa kuwa yupo pale kutoa huduma na si kunyanyasa wateja. Toa kwanza biriti kwenye jicho lako DAWASCO....

    ReplyDelete
  2. DAWASCO, MIMI NA WATANZANIA WENGINE AMBAO MMEELEKEZA MALALAMIKO YENU DHIDI YA HAO WADAIWA MNATAKA TUWASAIDIE VIPI? OFISI ZAO MNAZIJUA SASA MNAOGOPA NINI KUWAFUATA BADALA YA KULALAMIKIA USWAZI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...