Leo, katika Maktaba ya Jiji la Dar-es-salaam ambayo pia ni Maktaba Kuu ya Taifa, Faraja Nyalandu ambaye ni Mkurugenzi katika taasisi yake ya Shule Direct amekabidhi kitabu chake kipya cha “Unaweza” kwa ajili ya wanafunzi watakaofika kwenye maktaba hiyo.
Kama jina la kitabu hicho, “Unaweza” ni kitabu kinacholenga kusaidia wanafunzi kujenga uwezo na maarifa ili kumudu masomo yao. Ili waende shule kwa malengo na sio tu kwasababu ni wajibu. Waweze kuelewa namna za kujifunza. Zaidi, wajue namna za kuelewa na umuhimu wa kujenga ufahamu.
Faraja Nyalandu amenukuliwa akisema, “Kitabu cha Unaweza, Mbinu Kumi za kumudu masomo yako, kilizaliwa kwa sababu nimeona kuna haja ya wanafunzi kuhimili changamoto za uanafunzi na kufanikisha vyema azma ya kwenda shule” “Tunajifunza kila siku, kuna wakati tunajua kwamba hapa sasa tunajifunza na kuna wakati hatujui kwamba tunajifunza. Ni muhimu kujenga misingi hii ya kujifunza mapema.”
Faraja pia amepongeza wanafunzi wote wanaotambua umuhimu wa kutumia maktaba, akisema ni mfano wa kuigwa. Aidha Faraja ametoa wito kwa watu mbali mbali wenye mapenzi mema na elimu kufadhili upatikanaji wa kitabu cha “Unaweza” kwenye maktaba nyingine za mikoa na wilaya.
Faraja amesema asilimia 50 ya mauzo ya kitabu cha “Unaweza” yataenda Chuo cha Ualimu cha Korogwe, hususan Chumba cha TEKNOHAMA kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu kwa kutumia teknolojia.
Faraja akimwonyesha mwanafunzi sehemu wa kusoma.
Faraja Kotta akiwa na Jacqueline Ntuyabaliwe.
Faraja Kotta akiwa na rafikiye Nancy Sumari
Mama Nyalandu,
ReplyDeleteAsante kwa kuonyesha mfano..... maarifa yaongezeka zaidi pale unapochangia ujuzi wako kwa wengine.
Hongera
ReplyDeleteHongera wadogo zangu,
endeleeni kuonyesha mfano wa yale ya kujenga, na si kubomoa maadili ya watoto wa Taifa hili!
Tuzidi pia kuwaombea hawa watoto wawe na bidii ya kusoma - maana kitabu hata kiwe kizuri vipi elimu iliyomo ndani yake haimsaidii mtu kwa kutizama cover...You girls know what I mean!