Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom
Tanzania, Matina Nkurlu akisisitiza jambo wakati wa Droo kubwa ya Mwezi ambapo
Bwana. Willison Urio (33) Mkazi wa Mbezi Beach Jijini Dar aliibuka Mshindi wa
Shilingi Milioni 20. Pamoja nae katika Picha ni Ofisa huduma za ziada wa kampuni
hiyo Mathew Kampambe na Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Chiku Saleh. Ili kushiriki katika Promosheni hiyo Mteja anatakiwa kutuma neno
PROMO kwenda namba 15544.
Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Chiku Saleh akihakiki namba ya Mshindi wa Milioni 20 wakati wakuchezesha
Droo kubwa ya Mwezi,kabla ya Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina
Nkurlu (katikati) kumpigia mshindi huyo ambapo Bw. Willison Urio (33) Mkazi wa
Mbezi Beach Jijini Dar aliibuka Mshindi. Anaeshuhudia ni Ofisa wa huduma za
ziada wa Vodacom Tanzania Mathew Kampambe. Ili kushiriki katika Promosheni hiyo
Mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.
*Shilingi Milioni 119 bado kushindaniwa
na Bodaboda 115
*Jumla ya bodaboda 315 na Tsh. Milioni 211
tayari zimetolewa
Huku siku zikiwa zinahesabika kwa
Promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kufikia
ukingoni, Neema imeendelea kuwashukia maelfu ya Watanzania na safari hii ni kwa
Bwana. Willison Urio Mkazi wa Mbezi
Beach jijini Dar es Salaam ameibuka Mshindi wa Shilingi Milioni 20.
Promosheni
hiyo ambayo imeboresha maisha ya mamia ya Watanzania Tangu kuanza kwake
imemuibua mshindi huyo ambae akizungumza kwa njia ya simu wakati alipopigiwa
simu akiwa mapumzikoni Mkoani Kilimanjaro alisema kupitia mchezo huo ameona
mwanga katika maisha yake kwani alikuwa akijipa matumaini kuwa ipo siku ndoto
yake itatimia.
“Maisha
ya sasa ni magumu sana na nivigumu kwa
mtu wa kawaida kupata kiasi kikubwa cha fedha kwa mkupuo, yaani ni vigumu
kuamini kwamba mtu unaweza kupata Milioni 20 kiurahisi tu, lakini leo nimeamini
kupitia Vodacom haya yote yanawezekana.
“Sasa
nimeona mwanga katika maisha yangu, nitajiendeleza kibiashara na kuhakikisha
ninakuwa na mafanikio na kuendelea kuwaunga mkono Vodacom kwa kuyabadilisha
maisha yangu” alisema Urio na Kuongeza.
Imekuwa
vigumu kwangu kuamini kama nimeshinda kiasi hiki cha fedha ninamshukuru sana
Mungu, Kuna siku nilisikia mama mmoja kutoka Arusha ameshinda milioni 10,
nilikaa siku zote na kujipa matumaini kuwa ipo siku nami nitashinda na sikukata
tamaa niliendelea kushiriki katika mchezo huu na leo nimejibiwa maombi yangu na
nimeona matunda ya kutokukata tamaa, alisema Urio.
Akizungumzia
juu ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina
Nkurlu amesema “mwitikio umekuwa mkubwa sana tangu tunaanza mpaka hapa
tulipofikia kwani watu wamekuwa wakijishindia bodaboda kwa ajili ya usafiri ama
kuanzisha biashara na pia fedha taslimu ambazo zimekuwa zikitumika kufanyia
biashara na matumizi mengine ya kimaisha.”
“Nia
ya Vodacom ni kuhakikisha inaboresha maisha ya wateja wake ambao wamekuwa
wakituunga mkono siku zote na kutufanya kuendelea kuwa namba moja, Tunawaahidi
tutaendelea kushirikiana nao na kuhakikisha tunaboresha maisha ya wateja wetu
kwa kuwaletea promosheni zaidi na zaidi.”
Nkurlu
aliongezea kwa kusema “mitaji ni kilio kikubwa cha wajasiriamali wengi nchini.
Kuunga mkono jitihada za wajasiriamali nchini kote ni lengo mojawapo la kampuni
yetu, hivyo tunaamini kwa bodaboda pamoja na fedha hizi tunazozitoa kwa
washindi zitasaidia kupiga hatua kibiashara na kuboresha maisha yao”.
“Ninawasihi
wateja wengine wa Vodacom waendelee kushiriki katika Promosheni hii ili nao
wapate mafanikio ambayo wengine wameyapata na wanayoendelea kuyapata kwani
mwishoni mwa mwezi huu watachezesha droo kubwa ya kupata mshindi wa Milioni 30”.
Alimalizia Meneja Uhusiano huyo.
Hadi
kufikia sasa zaidi ya watu 315 wamejishindia pikipiki”bodaboda”huku jumla ya
fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 211 zikiwa tayari zimekwisha tolewa
kati ya Milioni 330. Huku Milioni 119 zikisubiria washindi.
Ili
kujiunga na promosheni hii wateja wote wa Vodacom wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...