….Shukuruni Katika Kila Jambo Maana Hayo Ni Mapenzi Ya Mungu Kwenu katika Kristo Yesu.
1 Wathesalonike 5:18
Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu wetu, kama Mtume Paulo anavyotukusha katika barua yake
kwa 1 Wathe 5: 18. Kwanza, hatuna budi ya kumshukuru Mungu kwa kutusaidia kuumaliza Mwaka 2013. Pili,
tuna sababu nyingi za kumshukuru Mungu kwa kutuingiza katika Mwaka Mpya, 2014. Haya yote ni mapenzi
ya Mungu kwetu.
Katika Mwaka 2013, tuliweza kuuona Mkono wa Bwana katika mambo mengi; kwa mfano,
Mungu alitusadia kutimiza umri wa miaka minne katika Ibada ya Kiswahili Columbus. Pili, 2013 tuliweza
kuuona Wema wa Mungu pale Ibada ya Kiswahili Columbus ilipofanikiwa kupata utambulisho rasmi ndani ya
KANISA la Kiinjili la Kilutheri hapa Marekani, kuanzia ngazi ya Sinodi mpaka makao makuu yake pale Chicago.
Kwa hakika, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu wetu kwa mafanikio makubwa ndani ya Umoja wetu.
Vilevile, katika Mwaka 2013 tuliweza kupata baraka ya ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadhamini
wetu, ambao ni kanisa la Gethsemane na kanisa la Ascension. Kupitia kwa watumishi wa Mungu, Mchungaji
June Wilknis na Mchungaji Tim Miller, tulifanikiwa kupata huduma mbalimahali; kwa mfano mahali pa
kuabudia, huduma ya mpiga kinanda, na huduma nyingine muhimu bila ya matatizo yoyote. Vilevile,
tulifanikiwa kupata huduma za kiroho, kimwili na kijamii pale tulipokuwa na mahitaji ndani ya Ibada ya
Kiswahili na ndani ya jumuiya yetu kwa ujumla.
Kwa hakika, tuliweza kuuona Mkono wa Mungu ukiwa katikati
yetu. Mwaka 2013, ulizidi kuwa ni mwaka wa baraka kwetu pale Mungu alipotupatia huduma za kiuchungaji
kwa karibu zaidi kupitia mtushi wake, Mchungaji Ipyana Mwakabonga. Tuliipotazama NEEMA ya BWANA
katika mambo haya yote, tuliweza kufungua vinywa vyetu na kumshukuru Mungu wetu, “Pamoja na Kwa
Umoja” tulisema Mungu wetu ndiye EBENEZA ndani ya Umoja wetu.
Wapendwa katika Kristo, Mkono wa Bwana umetusaidia kuuona Mwaka Mpya, 2014. Pamoja
na kuendelea kutoa shukrani zetu kwa Mungu wetu aliyetutoa mbali na kutufikisha katika Mwaka 2014,
tunamuomba kila mmoja wetu aendelee kuumbea UMOJA wetu pamoja na huduma ya Ibada Ya Kiswahili
Columbus. Karibuni tuitangaze Habari hii Njema ,“Pamoja na kwa Umoja,” Habari Njema ambayo Mungu
ametutendea ndani ya JUMUIYA yetu.
Habari Njema iletayo furaha pale penye huzuni. Pamoja na kwa Umoja
tuwe NURU ndani na nje ya jumuiya yetu . Nuru iletayo Mwanga. Mwanga wenye kuleta matumaini mema
kwa watoto wa Mungu. Haya yote yatawezekana kwa IMANI , kama tunavyokumbushwa na nabii Jeremia, “ …
nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Yer.33:3.
Mwisho, tunamuomba kila mmoja wetu awe huru kutoa maoni au ushauri utakaoiboresha huduma
ya “Ibada Ya Kiswahili Columbus” katika Mwaka 2014. Karibuni sana ili tuweze kuujenga Mwili Kristo, “Pamoja
na kwa Umoja” kwa njia ya vipawa vyetu au karama zetu ambazo Mungu amembariki kila mmoja wetu. Mtunzi
wa Zaburi ya 133, anatukumbusha ujumbe ufuatao: …..Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu
wakae pamoja, na kwa umoja. Wapendwa katika Kristo Yesu, Mungu wetu anatupa mwaliko wa kuuanza
Mwaka 2014 tukiwa “Pamoja na kwa Umoja” na Mungu wetu. Mwaka 2014 na uwe mwaka wetu “PAMOJA
NA KWA UMOJA.” AMEN.
Mch. Ipiana Mwakabonga


.bmp)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...