Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean-michel Louboutin kushoto akimkabidhi Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamdam Omari Makame nishani ya heshima wakati walipokutana kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo mjini Lyon,Ufaransa.
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
SHIRIKISHO la Polisi wa Kimataifa Duniani INTERPOL, limesema litaendelea kuunga mkono juhudi zozote
zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha na kudumisha hali ya usalama wa Visiwa vya
Zanzibar kwa lengo la kuimarisha utalii kwenye eneo hilo.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean-
michel Louboutin, wakati alipokutana na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamdani Omari Makame,
aliyetembelea Makao Makuu ya Shirikisho hilo mjini Lyon Ufaransa ambapo walijadili mambo
mbalimbali ya kiusalama yanayoigusa Zanzibar kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Bw. Jean-michel amesema ipo haja kwa jumuia nyingine za kimataifa kuunga mkono juhudi za Tanzania
katika suala zima la kuimarisha usalama wa eneo hilo lenye historia inayovuta watalii kutoka katika
Katika ziara hiyo ambayo ililenga kuimarisha usalama wa kikanda, Kamishna Hamdani alisema kuwa
Jeshi la Polisi nchini Tanzania litaendelea kutoa msukumo na kushirikiana na Interpol ili kusaidia katika
mapambano ya uhalifu wa kimataifa.
Kamishna Handani ameutaja uhalifu ambao ni kero na kikwazocha uchumi kuwa ni pamoja na Ugaidi,
Uharamia, Biashara haramu ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine unaovuka mipaka.
Kamishna Hamdani ambaye amekabidhiwa nembo maalum ya Interol, pia alipata fursa ya kutembelea
vitengo mbalimbali vya Makao makuu ya Interpol na kupatiwa muhtasari wa mafunzo yanayotolewa na
Interol katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji Maafisa na Askari wa kada mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...