Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto) akikabidhi nakala
za Rasimu ya Katiba kwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Neville Meena (katikati) wakati wa
mkutano baina ya Tume hiyo na Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar esa Salaam leo Alhamisi Januari 2, 2014. Anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji
wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto) akikabidhi
nakala za Rasimu ya Katiba kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw.
Kajubi Mukajanga wakati wa mkutano baina ya Tume hiyo na Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF)
uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar esa Salaam leo Alhamisi Januari 2, 2014.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ( wa pili kulia) akizungumza
na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa mkutano baina yake ya Jukwaa la Wahariri
Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 2.
2014. Wengine Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga,
Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu Augstino
Ramadhani.
(PICHA NA TUME YA KATIBA).


Inapokuja issue ya serikali tatu kwenye Katiba mpya, Jaji Warioba simuelewi kabisa...
ReplyDeleteAnasema issue ya serikali tatu imetokana na maoni ya wananchi na wala siyo yeye, wala tume.
Lakini hapo hapo anaelezea jinsi ambavyo serikali tatu zinaweza fanya kazi,na kusisitiza kuwa siyo mzigo. Kitu ambacho naamini kabisa mwananchi kama mimi siwezi chambua na kutoa maoni jinsi serikali tatu zitakavyofanya kazi. Haya ni maoni ya tume.
Kuna kitu Warioba hajatuambia....
Tume ndiyo sasa imechukua jukumu la kuwashawishi watu wakubali serikali tatu....Juzi nimemsikia warioba anasema kama tunaweza anzisha wilaya au mikoa mipya kwa nini tushindwe anzisha serikali tatu....?
Naamini Bunge la Katiba litakuwa makini kwa hili..
Mh Warioba anataka kuleta confusion kwenye nchi kwa hili la serikali tatu..!ninaomba aeleze je muundo wake utakuwaje?ni raisi mmoja na makamu wawili?au maraisi watatu?sijawahi ona nchi moja ina marais watatu..!je hao wananchi waliulizwa muundo wake utakuwaje?au uwepo ulaji wa tume nyingine kupata maoni ya muundo wa serikali tatu?
ReplyDeletepia huku kusema ni maoni ya wananchi its not correct..wananchi wanaoua watuhumiwa kwa kuwachoma moto bila kuwapeleka polisi, wananchi wasio chimba vyoo mpaka serikali iwalazmishe,etc ni wananchi ambao si kila wanalosema utalichukua kama lilivyo!..kuwa na serikali nyingi ndani ya serikal moja kuna hitaji wananchi wenye high level of understanding ambapo kwa sasa wa-tz asilimia kubwa hawajafikia huko!.nchi zenye mfumo huo kama USA wananchi ni waelewa sana!
Mh. warioba tafadhal sana be realistic na usiongee nadharia maana mambo kama haya yanaweza ingiza nchi kwenye uvunjifu wa amani. Tumeona nchi nyingi africa ambapo uelewa wa wananchi wengi ni mdogo vitu vidogo tu wameishia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe!
mdau UK
Warioba ktokea mwanzo alishasema kuwa serikali tatuna leo hii anarudi kwa kusema maoni ya watu. je wao wananchi walisemakuwa wantaka serikali tatu walipata wapi kujua faida au hasara za serilaki moja, mbili (ya sasa) na tatu mpaka wakaona kuwa tofauti za zote ni kuwa serikali ya tatu ina faida na maendeleo ya watu. Hii kwanza kuongezea mzigo wananchi maana viongozi watakuwa wengi na wizara nyingi pamoja na matumizzi mengi ya serekali tatu na pia kusahahu mabunge matatu. hata kwenye dini inasema mvulana anapotaka kuwa na urafili na mwanamke lazima waowane na kuwa kitu kimoja, tizama ulaya wao sasa wanataka kuuganana kuwa taifa mooja kwa kila kitu na sisi tayari tupo pamoja na je kama anaona serekali tau ndio muhimu kwa watu mbona hajatoa malelezo kuhusu sheria za nnchi kama uraia, uongozi au madaraka ya viongozi kama marais wa tatu kwa ajili hii je kama zenji wakitaka kuwa nchi ya kiislamu na wantaka sheria za kislamu muungano hataweza kuzuia kwa mfano tizma russian ya zamani baadaya ya kutengana kwa kuwa na sehemu nyingine kutangaza kuwa nhchi je maendeleo gani walipata kwa maoni yangu napenda serikali tatu lakini kwa hali halisi na maendeleo ya sasa sio kuwa muhimu na pia ni hatari kwa tanzania. warioba ana lake na anaitakiwa nchi baya maana haya sio kueleta maendelo ya vizazi vijao bali ni kuwapeleka mabaya.
ReplyDelete