Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM,  imefanya kikao cha siku, Januari 13, 2014 mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete na kujadili mambo kadhaa ikiwemo kumteua Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa kiti cha Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Zanzibar na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mgombea huyu wa CCM kesho, Jumanne, Januari 14, 2013, atachukua fomu za tume za kugombea.

Nape amesema uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Gharib Bilal.

"Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi", alisema Nape na kuongeza;

Mahmoud Thabit Kombo
"Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili na Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu".

Nape alisema, pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu pia imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanikisha sherehe zake kwa ufanisi kutokana na maandalizi mazuri.

Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana CCM kwa kupata mgombea wenu, Kila la kheri Mr Mahmoud na Allah atakusimamia ushinde kiti hicho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...