Naitwa Cyril August Chami (PhD) Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini na Mjumbe wa NEC-CCM kupitia Wilaya ya Moshi Vijijini.

Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na mtu au watu waliotengeneza akaunti kwa jina langu kwenye  Mtandao wa Kijamii wa Facebook na kujifanya yeye au wao ndio mimi.

Wamepachika hata picha zangu zinazopatikana kirahisi kwa sababu ya majukumu ambayo nimeshawahi kuwa nayo kama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, na Waziri wa Viwanda na Biashara.

Hilo lenyewe, yaani kutengeneza akaunti kwenye Facebook kwa jina la mtu na kuweka picha zake bila ridhaa yake, ni kosa la jinai.

Lakini ubaya zaidi ni kwamba mtu huyo au watu hao wanawasiliana na wapiga kura wangu kule Moshi Vijijini na walio nje ya jimbo na kuwauliza kero zinazowakabili. Wanawajibu hao wananchi kana kwamba wao ndio mimi. Kwa vile wao sio mimi, majibu yao siyo sahihi. Lakini kwao hilo halina tatizo maana nia yao ni kunichafua.

Wanaenda mbali zaidi na kukitukana Chama changu cha Mapinduzi wakionyesha kuwa mimi ni shabiki na/au sympathiser wa CHADEMA.  Wanatukana wanachama wenzangu wa CCM na kwa maana hiyo, viongozi wangu wa CCM.

Naamini wanajua kuwa nia yao hii ni ovu lakini nawaomba watambue kuwa hawatafanikiwa katika malengo yao kwa sababu mtetezi wangu ni mkubwa kuliko nia hiyo yao.

Siyo siri kuwa asilimia kubwa ya mawasiliano kwenye mitandao yanafanyika kwa anwani feki, hivyo wajue kuwa hata wasomaji wangenishangaa sana kama ningejiundia akaunti ya Facebook,  niweke picha zangu, halafu NIANZE KUWATUKANA VIONGOZI, WANACHAMA NA CHAMA CHANGU CHA MAPINDUZI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pole sana Doctor.Ndiyo maana Uchina(mwaka 2009) walizuia Face Book,Twiter na nyinginezo walizoziita "politically sensisitive" links.Ni mwaka jana tu wameruhusu kaeneo kadogo ka Shanghai kutumia FB.TCRA kazi ni kwenu

    David V

    ReplyDelete
  2. Kiongozi! inasikitisha sana kusoma hiyo habari, la msingi ni kukomesha kwa kupeleka watu hao mahakamani ili iwe ni funzo kwa wengine. Haki huru za uandishi sio sababu ya kuvunja haki za binaadamu au kupotosha jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...