Katibu Mkuu wa Chama cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambap wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo ukumbi wa Mtenda,Soweto jijini Mbeya.
 Waendesha Bodaboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya,wakiwa wamembeba Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kuzungumza nao mapema leo jioni ndani ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya.
 Waendesha Bodaboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya,wakiwa wamembeba Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kuzungumza nao mapema leo jioni ndani ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya.
 Baadhi ya Waendesha boda boda wafurahia jambo kwenye mkutano huo
Waendesha Bodaboda wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye wakati wa mkutano huo.
Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza wakati wa mkutano na Waendesha Bodoboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema ambaye ni Mlezi wa Bodaboda Mkoani Mbeya,kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na Waendesha Bodaboda wa mjini humo,ambapo Wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la Polisi na Polisi Jamii katika kulinda Usalama wa Wananchi,wao wenyewe na mali kwa ujumla ,Changamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na Utulivu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Naomba nitumie nafasi hii kutoa machache yaliyo kichwani mwangu kuhusu nyie waendesha bodaboda kote Tanzania.Nawapenda sana,naheshimu sana kazi yenu.

    1:Jitahidini sana kuwasha taa zenu za mbele mnapokuwa barabarani muda wote(Nadhani ni sheria hii) iwe mchana au usiku.Mimi(sijui waendesha magari wengine) nikiwa naendesha gari naiona(spotting) kwa haraka sana pikipiki iliyowasha taa kwa mbali iwe kwa mbele au nyuma kuliko ile ambayo haijawasha taa.Kwa madereva wengi,bodaboda "HAZIONEKANI" ndiyo maana nashauri taa kubwa ya mbele iwashwe muda wote.

    2:Overtaking:Kulipita gari lililo mbele yake jitahidini sana kupita upande wa dereva alipo.Kwa Tanzania asilimia kubwa ya magari usukani upo upande wa kulia,jaribuni kulipita gari la mbele yako kupitia upande wa kulia w gari.Gari lina vioo vya pembeni(kwa dereva kuangalia nyuma ya gari) viwili,lakini kiukweli madereva wengi wanaangalia sana kioo kilicho upande wao kuliko kile kingine cha upande mwingine.Wewe unayepita upande mwingine wa gari unahatarisha maisha yako!.

    3:Madereva-Mwendesha bodaboda,mtembea kwa miguu,mikokoteni,baiskeli nk.wana haki ya kutumia barabara,waheshimiwe ingawa barabara zetu si nzuri sana.Nilitembelea China,bodaboda zipo na madereva wa magari wanawajali,wanawaheshimu sana waendesha boda boda na watumaiaji wengine wa barabara tofauti na Tanzania.TUPUNGUZE AJALI ZA BARABARANI TANZANIA MWAKA 2014!

    David V

    ReplyDelete
  2. Hapo umenena kweli,ni vyema kutumia fursa kama hizi kuelimisha zaidi kuliko kutumia mda mwingi kwa kampeni,vilevile mhamasishe waendesha bodaboda kuwa na helmet za wateja wao pia.

    ReplyDelete
  3. Bodaboda zimekuwa mtaji muhimu sana kwa maisha ya watu na siasa za nchi hii.

    sesophy

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza:

    Mantiki ya Katibu Mkuu wa Chama kuonana na hawa Vijana ni kuwapa mwamko ya kuwa wasikubali kirahisi kutumiwa na wanaotafuta Uongozi wa juu nchini kuelekea 2015 kama ulivyoona Taarifa za vyombo vya habari wiki hii!!!

    ReplyDelete
  5. Kweli kabisa Mdau wa Kwanza kwa maoni yako juu ya Bodaboda kuzingatia Kanuni za Usalama barabarani!!!

    Pia ni vema wakazingati sana hizi kanuni na kuacha kutumika Kisiasa kupendekeza Wagombea Uraisi 2015 kwa ahadi ya kupewa Mikopo ya Pikipiki, kwa kuwa Taratibu za kuwapata Wagombea Uraisi na Uongozi hapa Tanzania zipo chini ya Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi nchini NEC na sio kwa Vijana wa Bodaboda!

    ReplyDelete
  6. Mdau David umesahau vifaa vya usalama kwa hizo bodaboda: kama pikipiki haina kinga ya mikonononi (wrist) na magotini, waendesha bodaboda inabidi wavae vifaa maalumu la sivyo baada ya miaka 15 mpaka 20 watashindwa kutembea hata kukunja ngumi. Helmet na jacket kifuani nimeliacha kwani linaeleweka. Ila wakiingiza uroho mimi hapo sipo (mfano mishikaki, au kuwa na haraka isiyo na tija)! Pia siasa zingekaa mbali kabisa na hawa watafutaji!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...