Juzi Kati ndani ya studio za Sibuka FM,Katika kipindi cha Pepeta Afrika, mgeni rasmi nyota wa wiki alikuwa kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi maarufu barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni,aka Anunnaki Alien au "Watoto wa Mbwa". 

Kamanda Ras Makunja alifanya maohijiano ya TV na Redio Sibuka, na alizungumuzia zaidi nafasi ya muziki wa dansi wa Tanzania katika masoko ya kimataifa, Mwanamuziki huyo wa Tanzania mwenye makao yake nchini Ujerumani alitoa wito kwa watanzania waishio ndani na nje ya Tanzania kuzipa nafasi bendi za muziki za Tanzania ili ziweze kuvusha muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania ,pia kufanya tour za kimataifa.

 Ras Makunja aliutaja muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" kuwa una nafasi kubwa katika soko la kimataifa hiwapo Watanzania wenyewe watakuwa mstari wa mbele katika kuutanga na kuzipendekeza bendi za Tanzania kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho ya kimataifa. 

Katika studio za Sibuka FM,jijini Dar-es-salaam Ras Makunja aliongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Komandoo Hamza Kalala ambaye aliutaja muziki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kuwa ni muziki ulipangiliwa kwa mtindo wa kushambulia na kuteka washabiki katika masoko. 

Komando Hamza Kalala alimtaja Kamanda Ras Makunja kuwa ni mojawapo wa wanamuziki wachache wa kitanzania wanao ipeperusha bendera ya Bongo kimataifa bila ya uwoga. Usikose kuwasikiliza FFU wa Ngoma Africa band at www.ngoma-africa.com 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Komando naona unapeana mkono na mkuu wa vikosi vya kutuliza ghasia nje ya nchi FFU ughaibuni
    kamanda Ras Makunja aka Field-marshal,mtawala wa himaya ya viumbe wa ajabu Anunnaki Alien ,

    ReplyDelete
  2. te!te!te! Kikamanda ketu Ras Makunja wa FFU Ughaibuni napokua uraiani mwanaadamu kamili ! anapokuwa jukwaani ni simba kichaa mwenye meno ya kutisha! kichaa wetu tunakukubali na kikosi chako FFU au Watoto wa Mbwa ni babu kubwa

    ReplyDelete
  3. chonde chonde kaka Kalala,huyo unaepeana nae mikono si kiumbe wa kawaida,ras makunja aka kamanda mkuu wa kikosi cha ffu ughaibuni,kolokoloni namba one,mtawala wa Anunnaki Empire,ndani ya Empire ya kunafugwa viumbe wa ajabu sana wakiwemo Bundi,Popo,dudumizi ! na siri ya himaya yake kubwa sana

    ReplyDelete
  4. HI! baba mtukutu kamanda ras Makunja upo Dar?
    unaonekana kama vile binadamu wa kawaida ! kumbe simba ndani ya ngozi ya kondoo, hongera baba kazi yako tunaikubali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...