NA RAMADHANI JUMA,KALAMBO

Zaidi ya Maafisa kilimo 40 wa wilaya ya Kalambo wanakutana kwa muda wa siku mbili katika kikao kazi kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kuinua uzalishaji na kuwainua wakulima wa wilaya hiyo ili waondokane na hali ya umasikini.

Kikao kazi hicho kinachofanyika katika kijiji cha Msanzi wilayani humo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa serikali wa "Matokeo Makubwa Sasa" katika sekta ya kilimo.

Akifungua kikao kazi hicho, Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a aliwataka Maafisa hao kuwa mfano wa kuigwa na wakulima wa wilaya hiyo kwa kuwa na mashamba yao yaliyolimwa kisasa.

Aliwataka pia kuhakikisha kila kata na vijiji wanakofanyia kazi kunakuwa na shamba darasa lenye ukubwa usiopungua robo eka kwa ajili kutolea mafunzo kwa wakulima, sambamba na utunzaji wa takwimu halisi kwa vpindi tofauti ili kuwa utendaji kazi wenye tija na unaopimika.

Aliwaagiza pia kusimamia kwa karibu utekelezaji wa kila shule ya msingi na sekondari wilayni kulima shamba lisilopungua ekari tano ili wanafunzi wapate uhakika wa chakula wakati wa masomo kwa lengo la kuinua kiwango cha ufaulu.

Mwishoni mwa mwaka jana, mkuu huyo wa wilaya alitangaza mpango wa kuzipatia shule zote wilayani humo vocha tano za pembejeo ili zifanikishe uzalishaji wa chakula cha wanafunzi wanapokuwa masomoni

Wilaya ya Kalambo yenye Kata 17 na Vijiji 100 ina maafisa kilimo zaidi ya 40 waliopo katika kata na vijiji hivyo.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akizungumza na maafisa ugani wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo alipofungua kikao kazi chao cha siku mbili jana katika kijiji cha Msanzi kata ya Msanzi wilayani humo.

Mmoja ya wawezeshaji katika kikao kazi cha maafisa ugani wa wilaya ya Kalambo Emmanuel Ebanks Lema (kulia) akifuatilia kikao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wilaya ya Kalambo iko wapi? Uandishi mwingine sijui tutafika lini!

    ReplyDelete
  2. Hivi wengine hawasikii? Ondoa hiyo label ya suti yako!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...