Na Andrew Chale, Zanzibar
CHAMA cha Mapinduzi CCM, leo Januari 24, kinatarajia kufanya kampeni yake ya tatu ya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Buyu Pwani, katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, ambapo mgeni rasmi wa kumnadi Mgombea anatarajiwa kuwa, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Jumuiya ya CCM (UVCCM) na (MNEC), Ndugu. Shaka Hamdu Shaka.
Akielezea mkutano huo wa tatu wa hadhara, unaotarajiwa kuwa majira ya Saa kumi jioni, eneo hilo la Buyu- Chukwani, Mahmod Thabit Kombo , aliwaomba wananchi wa Buyu kujitokeza kwa wingi ilikumsikiliza na kuzijua sera za Chama katika kuwaletea maendeleo.
“Leo Januari 24, nawaomba wananchi wa Buyu, kujitokeza kwa wingi ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu tuliyojipangia ndani ya chama” alisema Mahmoud Thabit Kombo.
Aidha, aliwaomba wananchi wa Buyu, ifikapo Februari 2, 2014 siku ya Jumapili, wampigie kura ya NDIYO, ili awe Mwakilishi wao atakayeenda kuwatetea kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza kero zinazowakabiri.
Baadhi ya mambo, mbalimbali anatarajia kuzungumzia ikiwemo kero za maji, elimu, kuwezesha vijana, akinamama na jamii nzima ya jimbo hilo la Kiembesamaki, pindi watakapomchagua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...