Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtambulisha mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Ilani Katiba na Sera ya CCM mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akihutubia wananchi na wanachama wa CCM kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika jana jioni 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
Mfalme wa Taarab Mzee Yusssuf na Mgombea Uwakilishi jimbo la KiembeSamaki CCM Mahamoud Thabit kombo wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi Jimbo hilo uliofanyika jana jioni 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
 Wananchi na Wanachama wa CCM Zanzibar wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika jana jioni 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.(Picha na OMR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. NAOMBA KUKIONGOZA KIKAO CHA KUMPITISHA MGOMBEA WA URAISI KWA TIKETI YA CCM 2015.

    Nimekuwa nikifuatilia sana siasa zetu kwa siku za hivi karibuni (ambazo kuna wengine wamezibatiza kama siasa maji taka/uchwara). Ni bayana kuwa sikuwahi kupiga kura kumchagua raisi wangu huko nyuma lakini hivi sasa hasa kwa kutambua umuhimu wa kura yangu na vile vile uzalendo wangu nashawishika kwa kiasi kikubwa kupiga kura katika uchaguzi ujao (yaani 2015).

    Kwa nanini basi imekuwa hivyo sasa?
    Kati ya matusi ambayo mimi huniuma sana ni mtu kutumia uwezo wake wa mali, fedha wazazi (family influence) kurubuni mtu au watu kwa lengo la kutimiza heshima yake binafsi. Haiyumkini na ni jambo lililo dhahiri kabisa kwamba uchaguzi ujao, narudia tena, uchaguzi ujao (wa kumchagua raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015), unaweza ukawa ni moja kati ya chaguzi ambazo pesa ya mtu binafsi au kikundi inaweza ikapindisha maamuzi kuliko chaguzi nyingine zozote huko nyuma.

    Mwalimu (hayati baba wa taifa letu, J.K. Nyerere) alitupa mwongozo mzuri wa kutoa maamuzi hasa tunapoelekea katika kipindi kama hiki. Kwamba,

    “...jamani eeeh! Watumiao gharama mbalimbali ili kuiona ikulu hawatufai ...watazirudisha vipi gharama walizozitumia kwenda ikulu pindi watakapo pata nafasi ya kuwa maraisi wetu?”

    Nasema, haihitaji digrii (au unaweza kusema shahada) ya chuo chochote kulitambua hili, kwamba kuna watu wamekuwa wakitumia gharama kubwa mno ili “kuweza kutimiza ndoto zao za kwenda ikulu”. Hii si tu ni hatari bali pia ni tusi kubwa kwa watanzania ambao wengi wao wamekuwa katika hali duni kwa muda mrefu, hali ambayo inahitaji uwepo wa sera madhubuti, endelevu na zinazotekelezeka ili kuwakomboa na wala si kusema “nitawapatia maji watanzania...” na vinginevyo.

    Tutambue kuwa nafasi ya uraisi ni wito na wala si kijiwe cha visasi na mahala pa kutimiza matakwa ya hulka zetu za kupenda “ukubwa” kwa sababu tumeouzoea. Uraisi/Ikulu ni taasisi/mahala ambapo mtu hatakiwi kupakimbilia isipokuwa kwamba ameguswa kwa dhati na mambo anuani ambayo anahisi akipata nafasi hiyo basi anaweza akatumia jitihada zake kuyarekebisha akishirikiana na watu watakaokuwa kwenye timu yake.

    Kwa mwenendo uliopo hivi sasa wa vyama vya siasa ni dhahiri kuwa CCM ndio chama au taasisi iliyo katika nafasi nzuri ya kuweza kutoa mgombea ambaye hatimaye anaweza kuwa ndio raisi ajae wa Jamhuri yetu. Nina hofu ... nina jaka moyo la dhati kutoka ndani ya utashi wangu kwamba viongozi wa juu wa CCM na hasa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa CCM wasipolilichukulia hili kwa umakini basi hawa watu wanaotaka “kutimiza ndoto zao” kwa asilimia 90 na za watanzania kwa asilimia 0.002 wanaweza wakapata kile walichokuwa wakipita kumwaga mihela kukiwinda. Na kama ndo hivyo basi ...

    NINAOMBA NIPEWE UWENYEKITI WA MUDA WA CCM WAKATI WA KIKAO CHA KUMCHAGUA MGOMBEA WA URAISI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI NA NINAAHIDI KUTUMIA VYEMA KADI YANGU KAMA NITAONA MAMBO HAYAENDI SAWA KWA KUSEMA ...,

    “...Abdul (Kinana, - Katibu Mkuu wa CCM), kama jina la ... lipo hapo, basi mimi narudisha kadi yangu ...!!”

    Ahsanteni.

    ReplyDelete
  2. Hapo juu, if you are serious you should have provided your name!! They will put whoever they want and they will win. Wabongo - why bother even going to vote - for me no, I have other things to do. Acha wale mwishowe watachoka na wengine watakuja. Nchi ya kuliwa hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...