Mweneyekiti wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola barani Afrika na Katibu wa Bunge la Ghana Bwana Emmanuel Anyimadu (kushoto) akifungua rasmi Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Umoja huo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika), mwenyeji wa Mkutano huo na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah.
Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) wakiwa kwenye Mkutano wa kamati ya Utendaji Jijini Dar es Salaam. Washiriki katika Kamati ya Utendaji wanatoka katika nchi za Ghana, Uganda, Tanzania, Botswana, Kenya, Afrika Kusini na Zanzibar.
Picha ya pamoja ya Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) pamoja na maafisa waandamizi wakati wa Mkutano wa Kamati ya Utendaji Jijini Dar es Salaam. Lengo la Mkutano huu ni kuandaa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Jumuiya ya Madola (Afrika) utakaofanyika nchini Kenya mwezi Juni, 2014. (Picha na Prosper Minja – Bunge)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Makatubu wanatoka nchi za "Ghana, Uganda, Tanzania, Botswana, Kenya, Afrika Kusini na Zanzibar"!!!!?????

    Hivi Serikali tatu tayari? Kumbe nchi mbili zipo njiani!!! Yetu macho! Historia twaiandika pole pole!!

    ReplyDelete
  2. mdau wa kwanza,si tatu tu.Bali nchi zote kujitegemea. Hivi ofisi zitakuwa wapi? Wazanzibar wana vyuo vingapi vya elimu ya juu? Iwapo mwanachama asipochangia kuendesha serikali ya muungano,je mawaziri wake watalipwa na nani?
    mmmmhhhh,hayeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...