Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini. Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo  wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
 Amesema uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu. 
 Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari 20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam. 
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hilo la wachezaji wa timu ya taifa kutoka kwenye timu tifautitofauti nimelipenda kila la kheri malinzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...