Mbunge wa Mufindi Kusini Menrad Kigola akizungumza  na mmoja wa watoto waishio katika mazingira hatarishi katika kituo cha itulituli.(picha zote na Denis Mlowe)
Mbunge wa Mufindi Kusini Menrad Kigola akiwa katika sherehe za mwaka mpya 2014 na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi jijini 
=========  ========  =========
NG’O WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA WATOTO YATIMA

Na Denis Mlowe,Mufindi.

WAKURUGENZI wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoanzishwa kwa lengo la kuhudumia jamii na hasa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu nchini wametakiwa kutimiza malengo ya uanzishwaji wa mashirika hayo kwa kuwanufaisha walengwa badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini (CCM) Menrad Kigola wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki 7 kwa kituo cha watoto yatima na wale wanaoishi ktk mazingira magumu wa kituo cha Ifulifuli kilichopo wilaya Mufindi mkoani Iringa na kuongeza kuwa kumekuwa na utitiri wa NGOs ambazo zimekuwa zikipata mamilioni ya pesa kutoka kwa wahisani lakini badala ya kuwasaidia walengwa waliokusudia pesa hizo huishia kuwanufaisha watu wachache kwa manufaa yao binafsi.

Kigola ambaye pia alipata wasaa wa kula chakula cha mchana na watoto hao kwa lengo la kuukalibisha mwaka mpya amewataka watoto yatima kote nchini kutojiona wa thamani ya chini kufutia maswaibu wanayoyapitia na badala yake kuwekeza muda wao mwingi kusoma hali itakayosaidia Taifa  kuwa na hazina kubwa ya wasomi ktk siku za usoni.

Alisema imekuwa ni kawaida ya baadhi ya asasi zinazolea watoto yatima kutumia misaada wanayopatiwa kwa manufaa ya waanzilishi kuliko malengo halisi ya asasi hizo.

“Kuna baadhi yenu mmekuwa mnaanzisha asasi kwa lengo la kuwanyonya watoto yatima hakika haimpendezi mwenyezi MUNGU kuwatumia watoto yatima kwa manufaa yenu” alisema Kigola

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho kinachomilikiwa na kikundi cha MPENDE JIRANI,Wilson Ngogi ameitaka serikali kupitia vyombo vyake kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kubaini mashirika yanayokwenda kinyume na sheria na taratibu za uanzishwaji wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...