Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe,Halima  Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa. (picha zote na denis mlowe)
Na Denis Mlowe,Iringa
MWENYEKITI wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Hai na Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee walishikiliwa kwa muda na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, kwa kosa linalosemekana  kuzidisha muda wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mgama wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
Kwa majibu wa  Mhe. Mbowe alisema jeshi la polisi walimshikilia kwa masaa mawili kwa mahojiano na mkuu wa kituo cha polisi na kisha kumwachia huru.
Akizungumza na wafuasi wa Chadema kabla ya kupanda Helikopta na kuelekea mkoa wa Pwani akiambatana na Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee aliwataka wananchama wa Chadema kuungana katika kukijenga chama bila hofu na kuwashukuru kwa kuwaunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi.
Alisema wakati wanajiandaa kuondoka alipata malalamiko kutoka kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya kuwa wamezidisha muda wa kufanya mkutano katika kijiji hicho.
Mhe. Mbowe alisema kuwa chanzo kingine ni baadhi ya viongozi wa kijiji kuwadanganya wananchi katika mkutano uliotakiwa kufanyika katika vijiji vya kata ya Ukumbi kuwa watakuwepo  wabunge na mwenyekiti wa chama katika mkutano  kitu kilichosababisha kuwepo na dalili za ugomvi.

“Jeshi la polisi limetuhoji kuhusu mambo hayo na baada ya kuwaeleza walituachia huru... ila wamesema wakituhitaji watatuita lakini makamanda naomba sana mjenge chama na nawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi” Alisema Mhe. Mbowe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Fata sheria bila shuruti.

    ReplyDelete
  2. People's Power!!

    ReplyDelete
  3. Dah! Wanasiasa bwana, ni pasua vichwa. Mbowe anajua sheria za nchi, lakini anaamua kuzivunja makusudi ili akikamatwa ionekane kuwa serikali ya chama tawala inamwonea. Tabia za aina hii ni moja kati ya matangazo. Wanajua kuwa wanapokamatwa kwa mahojiano magazeti yao na mengine yataandika. Sisi wananchi tuzielewe janja za wanasiasa kuwa kila wakifanyacho ni matangazo kwao ili tuwahurumie na kuwapa kura zetu. Siku hizi hahurumiwi mtu wala kupewa mtu kura kirahisi hivyo hapa.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...