Wawakilishi wa Kudumu kutoka nchi 193 wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon wakati alipolizungumza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa. Alitumia fursa hiyo, kuainisha vipaumbele vyake vya mwaka 2014, mafanikio na changamoto zinazoukabili Umoja wa Mataifa ikiwamo migogoro inayoendelea huko Sudan ya Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na kwingineko Duniani. Akatahadharisha kwamba kama Jumuiya ya Kimataifa haitakuwa makini kuna hatari kubwa ya kutokea mauaji makubwa ya raia kama ambavyo imeshawahi kutokea huko nyuma.
Home
Unlabelled
MGOGORO WA SUDAN YA KUSINI UNATISHA - BAN KI MOON
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
'CoW' Kazi kwenu Msala ndio huo unaendelea kuchanika!
ReplyDeleteSudani yaKusini hali tete, si ndio ninyi Kenya ,Uganda na Rwanda mlikuwa mnalazimisha bila kutimiza Vigezo Sudani Kusini ipewe Uanachama EAC?
Kuacha ukabila, udini na ubabe wa kisiasa ni somo linalotokana na matukio ya Southern Sudan na Central African Republic.
ReplyDelete