Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao na watumishi wa idara ya afya wa hospitali kuu ya Mkoa iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga. Alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero, malalamiko pamoja na ushauri kwa ajili ya kuboresha huduma na utendaji katika hospitali hiyo. Kero mbalimbali zilitolewa ikiwepo upandishwaji wa vyeo kuchukua mda mrefu, kubadilishiwa muundo wa vyeo na kusababisha kupungua kwa mishara kimakosa, uhaba wa vitendea kazi pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji ambapo kwa sasa hamna hata mmoja.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla akifafanua baadhi ya mambo ya kiutawala katika kikao hicho. 
Wajumbe katika kikao hicho.
Mmoja ya wahudumu wa afya akitoa kero yake.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ankal mithupu una ubia na huyu mama?

    ReplyDelete
  2. afisa alievaa suti ya kijivu kwenye picha ya kwanza, inaelekea yuko kwenye face book wakata mkuu wake akitoa hotuba. chunga!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...