KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),Bwana Jumane Sagini akiongea na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya kusainiwa mkataba wa kusimamia mradi wa mabasi yaendayo haraka kati ya Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) na Kampuni ya Uholanzi ya REBEL Group jijini Dar es Salaam jana. Wengine kulia ni Kaimu Afisa Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo na Mshauri wa Masuala ya Fedha wa REBEL Group, Bw.Jeroen Kok (kushoto).
Kaimu Afisa Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo(kulia) akibadilishana nyaraka za makubaliano na Mshauri wa Masuala ya Fedha wa REBEL Group, Bw.Jeroen Kok (kushoto) muda mfupi baada ya kusaini mkataba jijini Dar Es Salaam jana anayeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),Bwana Jumanne Sagini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Inafurahisha hawa watoaji misaada wanapohakikisha hela zote zinarudi kwao.

    ReplyDelete
  2. Bora zirudi kwao kuliko zitue mikononi mwa Mafisadi matokeo yake tunaweza jikuta tunakatiwa Misaada bureee,,,wakati Mafisadi watajengea ma Baa, ma Pub na Maghorofa yao ya kukaa na familia zao.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza bora iwe hivyo,

    Hukumbuki Norway ilitudai Mafungu ya Fedha za Misaada yao kwa miradi kutotekelezwa?

    Si, unaona Uganda inavyo pumulia mashine kwa kukatiwa Misaada?

    Afadhali Holland , Wadachi wamekuja kisimami wenyewe ili tusije laumiana baadaye!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...