Hello mimi ni mtanzania niishie Kuwait City, Kuwait. Kampuni ninayofanyia kazi inataka kuniamishia Calgary, Alberta(Canada). 

Bahati mbaya sijawahi kufika Canada. Naomba kama kuna mtanzania yuko huko au aliwahi kukaa huko tuwasiliane kupitia email: tzasheesh@gmail.com. Nitashukuru kupata msaada kutoka kwenu mlioko Calgary.


Shukrani
Mdau Asheesh

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Nakushauri rudi nyumbani tujenge nchi yetu. Sio unakomaa kujenga nchi za watu. acha uoga,home sweet home hai hitaji kujiuliza.

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu umeokota Gold mwana sikudanganyi achana na huyo wa juu hapo iyo sehemu hakuna wageni wengi pazuri sana na kuna kazi sana mimi nakutakia mazuri kuna warundi wana pesa sana wabongo siku zote wana taka kwenda miji mikubwa kuzaa sur hawana pesa mwana dah wewe umenisuuza roho hako kamji kazuri sana kuna mafuta watu wa kule wana pesa wewe nenda acha ujamaa watakupa majungu na kuludishana nyuma eti ludi nyumbani kajenge nchi sasa kakuona wewe una ukifanya kazi huko utakuwa unabomoa nchi dah fikra nguma kuna watu pasua kichwa mwana mi nakushauri achana na kutafuta mtu wa kuwa nae wewe nenda kale bata hauto sahau hii nakupa maisha ya mbele kupiga kazi na kutuma mpunga bongo

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu, sio kila mtu ana bahati ya kurudi huko nyumbani akabahatika na kazi, jamaa ana bahati ana kazi nzuri kwa nini arudi nyumbani, kama wewe umebahatika huko basi jenga hiyo nchi, umejawa na wivu tu. Huna la maana la kuandika sio lazima uandike kitu kuna vitu vingi sana vya kufanya kuliko kutoa ushauri wa kipuuzi, ndio home sweet home lakini kama hujabahatika na kazi huko urudi tu mlundikane hapo??

    ReplyDelete
  4. Kuna chama cha watanzania, na mwenyewe kiti. Siku hizi kila kitu kwenye google, calgary ni pazuri kabisa,nnenda kajifunze mengi tu...Tanzania haiondoki tupo tu.

    ReplyDelete
  5. Mdau Asheesh jitayarishe na baridi kwani huko baridi kweli kweli. Kila la Heri!

    ReplyDelete
  6. Mi nimejaribu sana kurudi nyumbani ila kazi za kupeana,dhuluma kwenye viwanja. Too much corruption. Tunapenda kwetu matatizo ndiyo hayo. Nyie wabongo mbona mkitumiwa no mwende western union hamkatai. Acheni kusema watu.

    ReplyDelete
  7. Karibu sana Calgary; baridi utapiga pamba watu tunaishi.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana! Huyo mdau wa juu anakuonea wivu. Yeye kajenga nini hapa Tanzania?! Sana sana majungu na wivu... Nenda kapige mzigo.

    ReplyDelete
  9. we unaesifia nchi za watu, acha kukandia bongo. Bongo kuzuri bwana. Maisha ya ugenini ni magumu sana kama huna mtu unayemfahamu. Bongo ukishuka tu kuanzia airport unapata wenyeji. Pesa hazina mwisho na hakuna hata mmoja aliyetosheka kwa pesa. RUDI BONGO MWANAWANI, ACHA KUTANGA TANGA NCHI ZA WATU

    ReplyDelete
  10. Mdau Asheesh,

    Kwa jinsi Uchumi wa Dunia ulovyoyumba nchi za Magharibi ikiwemo (North America) Canada na Marekani ni bora ungebakia Arabuni ukala Tende na Maziwa!

    Huwezi amini, nchi kama Canada watu wamchoka kimaisha, labda angalau wale waliosoma sana wakaajiriwa ktk Mashirika makubwa duniani ama Serikalini Canada ndio wana afadhali.

    Pana Watanzania ktk miji mbali mbali hapo CA wanafanya kazi za (vipato vya chini) kama walizo kuwa wakifanya wakiwa Bongo kama:

    -Kuuza Magazeti,
    -Kuuza Chapati na Maandazi
    -Ukorokoloni (Ulinzi Madukani)
    -Kuuza Kete za Madawa ya kulevya
    -Uweita kwenye Migahawa

    Huku wengi tu wakifanya matengenezo ya Masinki na mabomba ya maji taka vyooni!

    Kwa ufafanuzi mfupi huo ni afadhali urudi Bongo KIKWETE ANA TOA MISHAHARA MIKUBWA ama ungebaki hapo hapo Kuaiti City, Kuwait kwa Waarabu ukala TENDE NA MAZIWA!!!

    ReplyDelete
  11. Huna sababu za kuwa Utumwani Ugenini ni vile Tanzania imeshapata mali kubwa sana GESI FUTI ZA UJAZO TRILIONI 43 AMBAZO ZITAFIKA ZAIDI YA FUTI ZA UJAZO 400 TRILIONI NA HAPO UZALISHAJI UKICHANGANYA RAISI KIKWETE ATAANZA KUGAWA MISHAHARA KWA WASIO NA AJIRA NCHINI TANZANIA (UNEMPLOYEMENT BENEFITS)!!!

    ReplyDelete
  12. ukirudi bongo itakubidi uwe makini na vidole vyako ili wasing'oe KUCHA KUNA ZANA MAALUM ZA KUNG'OLEA KUCHA.HAYA WE MWENEWANE.

    MDA OHIO, USA.

    ReplyDelete
  13. njoo kijana ila baridi la huku canada we acha tuu.. summer uko wapi eeh

    ReplyDelete
  14. Mdau Asheesh,

    Mambo yamebadilika sana siku hizi sio kama siku zileee!

    Kurudi nyuma miaka ya 2000 ilikuwa (MAJUU, ikiwemo hiyo CANADA) MAJUU ILIKUWA NI MAJUU HASWA, na kuwa huku Tanzania na nchi zingine kulikuwa MACHINI LAKINI TOKEA UCHUMI WA DUNIA ULIPO ANZA DALILIZA KUTIKISIKA KUANZIA MIAKA YA 2000 KUJA JUU HADI KUFIKIA KILELE 2008 NA MAMBO YALIBADILIKA!

    IMEKUWA KAMA GWARIDE KAMA LILIPIGWA ZANZIBAR JANA KWENYE KILELE CHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI, NI KUWA:

    KWA SASA,

    MAJUU (Marekani, Canada na Ulaya) imemiwa MACHINI, n huku MACHINI(Tanzania, Asia na Afrika) kumekuwa ndio MAJUU!...NI KAMA GWARIDE KAMANDA ANAPOSEMA NYUMAAA GEUKA WA MBELE ANAKUWA NYUMA NA WANYUMA ANAKUWA MBELE!

    Juzi kwenye Operesheni Kimbunga tulistaajabu ya Mussa tulipoona Raia wa nchi kama NORWAY, ITALY, GERMANY NA DENMARK wananaswa na Kinbunga cha Raisi Kikwete!,,,haoa ndio kuthibitisha ya kuwa kwa sasa TANZANIA IMEKUWA NI MAJUU!

    HUWEZI AMINI WATU WANACHUMA FEDHA NA KUTAJIRIKA KWENYE NCHI KAMA MSUMBIJI NA SIO MAJUU,,,UNAWEZA AMINI? BASI HABARI NDIO HIYO!!!

    WALA USIHANGAIKE KWENDA CANADA UTAKWENDA KUFANYWA KULI NA KUBEBESHWA MABOKSI!

    NEEMA IMEFUNGUKA TANZANIA, RUDI KAMA ULIKUWA HUNA KITAMBULISHO CHA TAIFA HARAKA UKIFIKA JISAJILI, TAFUTA KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA NA VINGINE VYA MUHIMU NA USUBIRI KIDOGO MFEREJI WA MAISHA BORA UNAKARIBIA KUTIRIRIKA KWA KUWA RAISI KIKWETE ANATAKA KUWAACHA WANANCHI MWAKA 2015 KWA KUTOA SHUKRANI ZAKE !!!

    ReplyDelete
  15. Ndg.Asheesh huko Kuwait:

    Maisha ktk dunia yetu yanakwenda yakibadilika sana siku hadi siku.

    Zamani zile miaka ya 90 kushuka chini mtu akisema Majuu ilikuwa Majuu kweli, achilia mbali Majuuu Ulaya na Marekani, sema mtu akisema Bondeni (South Africa) ilikuwa ni kama Mamtoni vile, lakini sasa dunia imeporomoka vibaya sana ikichangiwa zaidi na Mtikisiko wa Kiuchumi wa Dunia hasa ilipofikia mwaka 2008.

    Nchi nyingi viwango vya maisha vimeporomoka sana duniani, unakuta watu waliopo nchi kama NORWAY , wanawaza kwenda MAREKANI, na waliopo Marekani wanawaza kwenda NORWAY ilhli kila mtu anajenga fikra kuwa sehemu zingine kuna unafuu Fulani kitu ambacho sio KWELI DUNIA NZIMA IMEPOROMOKA , afadhali AFRIKA uwezekano upo kwa kuwa watu wangali wamelala hivyo ni rahisi kupiga mabao na kufanikisha kama jinsi Wahamiaji haramu wanaitumia nafasi hiyo nchini Tanzania, unakuta Mhindi anaingia kinyemela akiwa Fala muda mfupi tayari kimeeleweka.

    Wala usifikirie kwenda CANADA kwa kuwa huko utakuta watu wanabeba Maboksi huku vipato vikiwa chini sana!, NI AFADHALI UFIKIRIE KUREJEA NA KWENDA ANGOLA AMA MSUMBIJI UTAFANIKIWA !!!

    Usijidanganye Majuu mambo yameporomoka sana miaka hii ukiacha miaka ile ya 90 na huko nyuma, wengi waliopo huko wanabakia huko na kuogopa kurudi Bongo huku wakiwa hohehae kwa aibu !!!

    ReplyDelete
  16. Mdau wa Kuwait, umeona Mdau wa No.15 hapo juu anakuthibitishia Raia wa nchi zinazoaminika zina maisha bora Duniani (Norway, Germany, Italy na Denmark) wanakamatwa ktk Operesheni Kimbunga ya Uhamiaji haramu nchini Tanzania?

    Kama kwao walikuwa wamehakikishiwa Maisha bora huku Tanzania kwa Kikwete walikuwa wanangoja nini hadi wanazidisha muda wa visa?

    Kwa hiyo Mdau wa Mchanganuo huu utajua kusuka ama kunyoa, (NCHI ZENYE VIWANGO VYA MAISHA KAMA HUKO CANADA WANAZAMA TANZANIA HADI WANAKAMATWA KWA UHAMIAJI HARAMU) la muhimu ujiamini chukua ndege Rudi Tanzania!

    ReplyDelete
  17. Paki mabegi yako rudi Tanzania!

    Usihangaike kwenda Canada kwa kuwa Raisi Kikwete ameifanya Tanzania imekuwa Majuu!, kama unavyona Mdau wa No. 15 akisema Wazungu kutoka Norway, Denmark, Ujerumani na Italy wanazamia Tanzania na Kushikwa ktk Operesheni za Wahamiaji haramu!,,,ile ile Tanzania mliyokuwa mkiicheka zamani.

    1.Hukuona mwaka jana 2013 Raisi Kikwete aliendesha Operesheni Kimbunga iliyomletea lawama kwa Maraisi wa nchi Jirani kama Uganda na Rwanda?

    Ni kuwa Raisi Kikwete alikuwa anajituma kujenga mazingira KUWAFURUMUSHA WAGENI HARAMU ili Fursa walizopora Wageni haramu nchini uje kuchukua wewe uliyepo ugenini huko Arabuni ukitumikishwa kikazi.

    HIVYO HUNA SABABU KUBADILI NCHI HUKO KWA HUKO UKIHANGAIKA BURE WAKATI RAISI WA NCHI YAKO AMEKUTUMIKIA KWA NAMNA HIYO.

    2.Hukuona mwaka jana 2013 Maraisi wa Dunia wamekanyagana kuja Tanzania?

    ReplyDelete
  18. Samahani kaka michuzi mimi natoka nje ya hoja kuna jambo limeniumiza kichwa,last week kuna clip nilitumiwa inayomuonyesha mama mtu mzima akiwa utupu maskini akidaiwa mchawi kutoka moja ya mkoa wa Tanzania,niliingiwa na huruma jinsi yule mama alivyokuwa anazomewa na anahangaika hadharani,hivi watanzania bado hatujatambua kuna kitu kinachoitwa"DIMENTIA" huwapata wazee wakifika umri Fulani,tubadilike jamani.

    ReplyDelete
  19. Usisikilize watu hapo. Wewe umehamishiwa kazi hivyo tayari una ajira. Canada ukifika chukua leseni ya gari, nunua gari baridi huioni tena. Ughaibuni wenye shida ni watu wasiokuwa na makaratasi.
    Mdau
    UK

    ReplyDelete
  20. Kiongozi Asheesh kama Tende na Maziwa vimekukinai Arabuni ya nini tabu?

    Rudi uje kuikuta mohogo kwa kachumbari na juisi ya ukwaju!

    Fungasha mizigo usihangaike na dunia RUDISHA MPIRA KWA KIPA No.1 JAKAYA KIKWETE !

    Ile unafika utakuta Jakaya Kikwete amekuandalia fursa kibao!

    ReplyDelete
  21. Hahahahahaha!!!

    Mdau wa 15 umenifanya siku yangu kuwa nzuri kwa kicheko!

    ''MAJUU (Marekani, Canada na Ulaya) kumekuwa MAMCHINI''

    Na ''MACHINI(Tanzania, Asia na Afrika) kumekuwa MAJUU!

    Haahahahaha! ulamalizia na GWARIDE LA SHEREHE ZA MAPINDUZI MIAKA 50 ZANZIBAR,,,''GWARIDE GEUKA WA NYUMA ANAKUWA MBELE NA WA MBELE ANAKUWA NYUMA''

    Kweli maneno umeyapanga!

    ReplyDelete
  22. Hivi kwanini wabongo tuko hivi? Huyu mdau Asheesh ameweka swali rahisi sana. Anaomba msaada kutoka kwa watu walio Calgary wampe direction.. Ila majibu yote hapo juu hakuna aliyemsaidia matokeo yake tunaanzisha mdahalo ambao binafsi naona hauna maana.

    I am sure anaelewa maisha Tanzania yakoje. Ila yeye amechagua kuishi nje, kwanini tujadili au tujibu hata swali ambalo hatukuulizwa??…. Tujitahidi kufikiri kabla ya kuongea

    ReplyDelete
  23. haturudi ng'o tutarudi tu, hapo rushwa na ufisadi,itakpo isha nakuwepo sera nzuri ya ulinzi wa raia na mali zao kwa ujumla.Tanzania kuna tabaka kubwa kati waliyonacho na wasiyo kuwa nayo watu wachini wanateseka sana.Nchi gani baaada ya miaka hamisini ya uhuru bado umeme shida, maji shida,matibabu shida, elimu shida, namengine mengi sana, semeni nyie wengine mlioko nyumba baadhi mnatuonea gere hata na wewe sasa hivi unayesema turudi tujenge nchi ungepewa hata chance ya kuja huku majuu kwa wiki moja tu, nadhani ungechizika kwa furaha ungekubali hata kabla mtu hajamaliza kukuuliza wewe wacha bwana tubebe mabox yetu ndio inatufanya kuwa na safari ya kwenda west union kila mara kuwatumieni hela hiyohiyo mnayoizarau kana kwamba nyie mnazo zaidi kumbe choka mbayatu.

    ReplyDelete
  24. Rais Kikwete aomba msaada kwa Serikali ya China sasa wewe ludi ufe

    ReplyDelete
  25. Wadau kwa kwenda nje ya mada. Mie nimemuelewa muulizaji, ni mtz na anafanya kazi kuwait ila anahamishiwa Canada na hiyo hiyo compony ambayo anafanyia kazi kuwaiti. So haendi kubeba box wala kubangaiza na siku mkataba wake ukiusha atarudi Tz, hii ni sawa na raia wa nchi moja wanapoenda nchi nyingine kufanya kazi, inaongeza ujuzi pia, sasa nyie kila mtu akiuliza swali ooh rudi bongo fursa kubao.
    Kwa fursa gani hizo ukitaka kufungua biashara uzungushwe kama nini, ukikemea ubovu wa viongozi wanakurestisha in peace, kukung'oa kucha, kazi wanapeana wao kwa wao.
    Acheni kila mtu haishi alivyochagua, ye kataka kujua watz wanaoishi huo muda kama huishi hapo bora nyamaza, sio rudi oooh rudi ooh wangapi wanerudi na kumewaahinda sababu ya ukiritimba?
    Wengi wa mnaotaka harudi msibishe mshajaribu sana kuimba visa mmenyimwa ndo mnataka kila mtu harudi mje kupigwa nae vumbi, mie niko tz, kaka yangu rudi ukijisikia huku ukiritimba mtupu, watu hawataki kazi wanakuja kazini kuchelewa, rushwa ndo husiseme na ole wako ufungue mdomo wako kukemea, wataupindisha hapo hapo.
    Michuzi sijatukana mtu, post my comment please.

    ReplyDelete
  26. Suluhisho la kumsaidia ndugu yetu aliyepo Kuwaiti ni kurudi nymbani tu!

    Hamuoni ya kuwa amekata tamaa na kukosa kujiamini kwa kubadili nchi moja kwenda nchi nyingine huko kwa huko?

    Anaondoka Kuwaiti anakwenda Canada, kote huko ni majanga juu ya majanga.

    Kuwaiti(Matabaka ya kimaisha) na Canada(Mshike mshike wa kimaisha) kwa kiwango cha Ukosefu wa Ajira wa 7% na Sera za kuwabada Wageni Canada usishangae jamaa anaweza kufika akiwa na Kazi ktk Kampuni yake iliyomhamishia Canada kutoka Kuwait ukakuta anapunguzwa Kazi!!!

    Hivi sasa nchi za Magharibi zina Sera za 'Job Entrenchment' (yaani kupunguzwa watu kazini) ili kwenda na FISCAL POLICY ni masuala ya Ki-ajira ktk Uchumi wa nchi, hivyo hawawezi kumkosesha kazi Raia wa Canada akabebe Mabkksi halafu Mgeni aliyeingia awe Ofisini, ni wazi wewe Mgeni tena Foreignor kutoka Kuwait utabeba Maboksi na M-Canada atakaa kwenye kiti cha kuzunguka Ofisini!!!

    ReplyDelete
  27. Naungana na Mdau wa 27 hapo juu, suluhisho ndugu yetu wa Kuwaiti rudi nyumbani tuje tulichape DONA LA KIKWETE KWA MBAAZI!!!

    ReplyDelete
  28. Hata mimi namuunga Mkono Mtoa Maoni wa 27 haiwezekani wewe Mgenki Mtanzania kutokea Kuwaiti ukae Ofisini mwenyeji abebe Maboksi?

    Hapo wewe Mtanzani mgeni kutoka Kuwaiti utazibua mifereji na kubeba maboksi na M-Canada atakaa kiti cha kuzunguka Ofisini.

    Hiyo hata Raisi Kikwete hawezi kukubali itokee kwake Tanzania, si ndio maana dhidi wa Wageni na Wafanyakazi Haramu ameendesha Operesheni Kimbunga?

    ReplyDelete
  29. Ok, kusema ukweli watanzania tunasikitisha...
    Inakuwaje mtu aulize moja kujumlisha moja ni ngapi ila majibu yawe mdahalo???? Kwanini tunataka somehow tumpangie mtu maisha?
    Kwani watanzania wangapi wanakaa nje, wana kazi nzuri sana, maisha yanaenda.. Hata kama angekuwa anaenda kubeba box, kachagua mwenyewe na wewe inakuhusu nini...tujitahidi sana kufikiri

    Simjui Asheesh, ila naona kama tunamchanganya na midahalo isiyokuwa na maana. Na ndo maana nchi yetu siku zote tumekuwa wagumu kujiendeleza, kwanini?? midahalo tuuuu

    Kaka Michu, please usiniweke kapuni sijatukana

    ReplyDelete
  30. Samahani ndugu Michuzi: mie naomba niende nje' ya hoja kidogo. Tuongeage vitu vya msingi humu, naona watu wanaropoka sana(wanajifuraisha). Mie ni Mtanzania damu na naipenda sana Tanzania na watu wake. Nasoma maoni ya watu wachache wanafafanisha Bongo na Canada au Marekani, hiki ni kichekesho. Ni sawa na kufafanisha Bongo miaka 100 nyuma na Magharibi wako miaka100 mbele. Ndiyo mtu unatakiwa ujipe moyo, ujisikie na tupende kwetu, lakini hapa mjadala haupo. Mfano,mtu wa kawaida umetoka zako Posta kazini, kwa vile foleni ni balaa umeamua kukatiza kwa mguu kupitia za jangwani mpaka Sinza. Unafika nyumbani, Sinza, hoi toka kazini, maji, yaani MAJI ya kuoga hamna, inabidi ununue, tena toka kwenye vidumu. Marekani unatoka zako kubeba box unaoga muda wowote, maji ya moto au baridi toka kwenye bomba(ni jambo la kawaida). Hebu tuseme tena, kale kamsemo ketu BONGO KAMA MAREKANI-ni ndoto ya mwenda wazimu, tuwaache utani mwingine jamani. Tutafute watu wengine wakujifananisha nao. Na sielewi ni wivu ghani wa kipumbavu ambao wa Tanzania tunafanyiana!? Tuamke Wafrica, Tuamke Watanzania.

    ReplyDelete
  31. Kaka mtoa mada nyumbani ni nyumbani yes ila usijedanganyika eti rudi jenga nchi hao waliopo nyumbanni na wenye elimu zao mbona hawana kazi na opportunities za kuijenga nchi? Wewe una kazi yako na maybe familia inakutegemea sasa ukirudi tz UNADHANI UTAWEZA KUWASAIDIA KWA NAMNA UNAYOWASAIDIA SASA?ISITOSHE NDIO NYUMBANI WANASEMA KAMA MAREKANI SIJUI KAMA CANADA MAMBO MENGI WANACOMPARE KWA AJILI YA MAGHOROFA,NYUMBA ZA STAREHE NA NYUMBA ZA WATU WANAZOJENGA ILA HATA HIZO BASICS NI TATIZO...MFNAO WAMETOA HAPO,MAJI,TIBA HOSPITALINI, FOLENI ZA KUKUFANYA HATA USIENJOY KWENDA KAZINI NA KUSPEND MUDA NA FAMILIA N,K MFANO HATA HAO WENYE KUJIONA WANAMAISHA MAZURI MTU ANALIBANGALOW LAKE LAKNI HATA KUFLASH CHOO NI SHIDA HAMNA MAJI , UNAENDESHA RANGE ROVER LAKO UKIPATA AJALI HAMNA AMBAULANCE NA EMERGENCY SERVICES ITAYOKUFIKIA WITHIN 10 -20MINS NA MWISHONI NI WASAMARIA WEMA KUKUVUTA NA MAYBE KUKUPA UKIWETE IN PROCESS BILA KUSAHAU WENYE NIKA YA KUIBIA WAKATI UKO KWENYE HALI HIYO etc etc PLEASE WE RESEARCH HUO MJI NA TUMIA RESOURCES ZILIZOPO ONLINE KUJIANDAA NA MAISHA YA NCHI/MJI HUO.KILA LA KHERI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...