Habari zenu wadau wa blog ya jamii na Ankal kwa ujumla.
Mie ni mdau mkubwa wa blog hii, ni maswali mawili matatu naomba mnisaidie.
Nataka niende/nihamie USA ( kuhusu mambo ya makaratasi msijali yapo fresh), mji ninaotarajia kwenda ni Lowell, MA ila mwenyeji wangu sio mtz ndo nikaona niulize humu.
1:line gani nzuri ya simu kupiga Tz ukiwa USA?najua kuna sky pe, viber and co ila sio familia yangu yote ina huduma hiyo.
2: Je, nikikata insuarance USA itanicover incase nikipata na janga kama binadamu mfano kifo, itanirudisha kwetu nizikwe in time au ni bora kabla sijaenda nipite ofice za NSSF weledi( kama sijakosea) nikakate insurance ya hapo?.
Nimejaribu muuliza brother google kuhusu miji ambayo haina high criminal record, ila majibu yake yananichanganya.
Acha niwe mkweli natarajia kufanya kazi kama assistance nurse, kuja kuwa nurse. Je mji gani mnanishahuri ni mzuri ukiondoa Houston( huu story zake umenichosha tayari).
Najua mengine nitajifunza baada ya kufika huko ila si vibaya wadau mkianza kunipa hints kabla sijakwea pipa.
Asante na Mungu hawabariki na asante ankal kwa kijiwe hiki.
Hongera kwa kazi yako. Kila mji una uzuri na ubovu wake lakini isikuatishe tamaa kwa ujumla siyo pa baya jiandae tu kwa baridi kali wakati wa winter. Kabla ya Obamacare insurance ilikuwa optional, na kutegemeana mkataba wako wa kazi pengine utakuta kazi inakuja na package ya insurance, inabidi ujue hizo detail, Obamacare ina vipengele vya penalty kama mtu hana insurance. Ukikata hiyo ya Nssf inagaramia kusafirisha muhusika akifika. Nadhani wana website yao. Kuhusu line ya simu walio wengi wanatumia prepaid calling cards na deal hazipo sawa, kwa maana kila card in mapromotion mbalimbali. Wengi huishia viber, whatsapp, tango n.k.na kwa sehemu kubwa inakidhi mahitaji ya walio wengi. Kila la kheri.
ReplyDeleteChicago
ReplyDeleteSwali la kwanza aisee kupiga simu hata utumie line gani ni ghali. Labda uhakikishe unawasaliana na watu kwa viber au whatsapp kwa kuwa ni bure. Kuhusu swali la 2 sijui aisee ila nahisi ukiuliza NSSF watakuwa na ujuzi zaidi. Kuhusiana na kiasi cha uhalifu inategemeana na sehemu unayoishi. Unabidi uwe mjanja sehemu yoyote unayoishi. Usikae karibu sana na wanapokaa masikini kwa kuwa saa zingine ndio wao wanaotembea na mabunduki kila saa. Ukifika uanze kutafuta kazi na kuhakikisha kwamba hata kama umepanga kwa hela nyingi unakaa hapo maana ni bora kuliko kulipa kidogo na kutokuwa salama.
ReplyDeleteMdau wewe kwea pipa tu, kama umemudu kuishi bongo na kwingineko, US utapeta tu. Nursing professional inalipa utapata kazi, ila ukifika usichague kazi maana inawezachukua muda kidogo kupata kazi haswa kama hawatatambua vyeti vyako, i.e., unawezaambiwa ufanye mitihani ya huko. Miji hatari ninayoijua mimi ni Camden (NJ), Detroit (MI), na Oakland CA. Nakushauri upite NSSF kabisa, sidhani kama kuna insurance ambayo iko specific kama ya NSSF. Karibu N.America.
ReplyDeleteMdau Canada
Njoo ohio sie wa tz tupo
ReplyDeleteMan up, nursing assistant? We get those in nursing homes
ReplyDeleteWho cares
ReplyDeleteNashauri uchukue ya NSSF kwani unaweza kuwa na insurance zaidi ya moja.
ReplyDeleteHii ya NSSF inaitwa WESTADI, itakusaidia wewe na familia yako huku nyumbani.
Kila la kheri
lowell kuko sawa inategemea unaishi upande gani wa lowell. usihofu watanzania wamejaa kibao ukija utajionea. mimi naishi fitchburg sio mbali na lowell. kuhusu bima ya afya usihofu mwenyeji wako atakuelekeza ukifika. kama ni ya kifo ukitaka kurudishwa nyumbani westadi hiyo ya NSSF ndio wengi tunatumia. Njoo mambo yatajinyoosha tu hongera
ReplyDeleteUkisema mambo ya makaratasi yapo 'fresh' unamaana gani?? Maana inaonekana haujawahi kudunda USA. Na kama ni hivyo, sheria nyingi zimebadilika, na inabidi ujue what's current. Mambo ya insurance yapo mengi, kwa vile una 'makaratasi', then hilo lisiwe tabu. Watu uwa wanakimbilia NSSF kwa wale wenye matatizo ya 'makaratasi' au wenye upendeleo wa kuzikwa huku bongo. Kuna wengine tayari wana 'makaratasi' na wameshakuwa raia wa Marekani, hivyo uzikwa huko huko Marekani.
ReplyDeleteKuhusu MA, jiandae na baridi. Na pia usiogope, maisha ya Marekani ni kujipanga, na kwenda kwa wakati.
Nenda Seattle, WA utakuwa karibu na Bill Gate, pia kuna rafiki yangu anafanyakazi Microsoft atakupokea kutoka TZ. Mdau usiwe na shaka madhali una viza, kazi ni kibao Ughaibuni. Ukiwa unapanga chumba usinunue vitu vya thamani ukaweka ndani maana ukiondoka wapangaji wenzio watakuibia. Tafuta liseni ya gari haraka sana. Pia usitembee na pesa nyingi. Nunua simu ya "Contract" kama una marafiki wengi USA. Uwe mpole kwa wenyeji wako (raia wa USA), hususan Wazungu. Jifunze kusema taratibu. Fanya kazi kwa bidii na haraka haraka maana mabosi wanakuangalia. Nunua gari mara moja ukishapata liseni. Karibu ughaibuni!!
ReplyDeleteMdau
UK
Hongera kwa kuchukua hatua ya maulizo kabla ya maamuzi.kulingana na utaalamu wangu wa masuala ya bima(insurance ) Nakushauri uchukue travel insurance ambayo ina manufaa mengi sana ukiwa huko na endapo utapata majanga na kuhitaji kurudi au matibabu yakinifu, hivyo kama mshauri tembelea www.mgentanzania.com au info@mgentanzania.com. Natumaini utapata suluhisho la mahitaji yako.
ReplyDeleteMdau
Max
Lowell ni mmoja ya miji iliyo underservered kwenye eneo la Greater Lowell.
ReplyDeleteKuna wacambodia na spanish wengi sana.pia wakenya wamejazana huko sababu ya kazi na shule za nursing.Kuna umass lowell na middlesex community college ambazo zina nursing programs.
kuhusu insurance kabla hujaanza kazi unaweza kuapply mass health kwa sasa wameiingiza kwenye obamacare...affordable care, unaweza kujaribu kuapply kabla ya kupata kazi.
Simu ziko nyingi tu ila usichukue simu za contract, zitakubana for a year or two.unaweza tumia line za pay as you go..walmart wanaziuza kwa bei fresh tu.
ukikwama unaweza wasiliana na mimi, naishi karibu sana na lowell via jay.jaliwa@gmail.com
kila la heri
mdau
North Mass
we hamia tuu mambo mengine yatafuata baadae
ReplyDeletenjoo southside chicago..pazuri tu kwani mie na Obama tumeishi hapa karibia maisha yetu yote
ReplyDelete