Kuna mdada wa miaka 18 Ambae amejifungua binti anaeitwa Maryam kwa bahati mbaya sana mtoto Huyo alipozaliwa hakua na sehemu ya kutoa choo kikubwa hali ya Kua kwamba sehemu hiyo imefunga. Kwa ujuzi wa ma daktari wa muhimbili wamemtoboa hapo ubavuni ili atoe choo kikubwa kwa njia hii.
Madaktari walimshauri mama mzazi kuwa mtoto huyo atafanyiwa operation wa kufungua njia ya choo kikubwa akifika mwaka na nusu. Sasa amefika umri na mama mzazi yupo kwenye hali Duni sana na Hana hela ya kumfanyia mtoto operation huo.
Nawaomba ndugu zanguni tumsaidie huyu mtoto, kwani hali hii Inaweza kumkuta mtu yoyote. Haya ni Maisha Yake nawaomba mjitokeze kwa Moyo mkunjufu tumsaidie huyu mtoto.
Kama Una msaada Wowote ule tafadhali nipigie mimi apa kwa kutumia number: +255719009004 au Kama upo nje ya Tanzania na umeguswa na hili na unataka kutoa sadaka yako tafadhali Tuma kwenye account yangu ya Barclays: Miss S.Yussuf sort code: 207103 acc: 73049328 pia unaweza kutuma njia ya wastern union.
Kwa mlikuwepo Tanzania hiyo number yangu ya TIGO PESA. Ahsante sanaa
KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI. MUNGU AWABARIKI SANA.
Inasikitisha sana, nilikuwa India majuzi na nilikutana na idadi kubwa ya vigogo wa serikalini ambao wameletwa huko kwa check-up au matatizo madogo sana huku wakitumia mamilioni ya shilingi za wavuja jasho. Wengi wao hulipiwa usafiri kwenye "business class" na huwekwa kwenye luxury hotels huko India. Matumizi hayo ndio sababu haswa ya kushindwa kwa serikali kuwahudumia wagonjwa kama huyu binti. Tuamke jamani tuanze kuuliza maswali magumu.
ReplyDeleteMdau,
Tanga
kuna mtoto wa jamaa ambaye nilikuwa namjua alikuwa na kesi kama hii , mwanawe alizaliwa hana njia kubwa wakamtoboa pembeni kama hivyo wakamwambia akifia umri wa miaka miwli hivi watamfanyia operesheni kufungua ile sehemu ya kaawaida , lakini baada ya kufanyiwa hivyo mtoto alifariki baada ya siku chache tu wakati yupo wodini muhimbili , ushauir wangu ndugu yangu tafuta michango zaidi umpeleke india angalao ,
ReplyDeleteKwani mama yake huyo mtoto hana simu?
ReplyDeleteInahitajika kiasi gani?
ReplyDeleteOperation sh ngap?
ReplyDeleteProblem kubwa ya Tanzania hakuna UWAZI KABISA.
ReplyDeleteWapo watu wengi sana Tanzania wenye uwezo wa Kumsaidia huyu Kijana apate matibabu mazuri.
Ila shughuli inakuja kwenye "UWAZI"
Yaani Hata huyu anayekusanya Michango au Misaada hana Information za Ghalama za Matibabu zinazo hitajika ila kukamilisha zoezi hili.
Nakuomba sana , tena SANA utembelee Hospitali za Upasuaji hapo Tanzania. Ili upate Ghalama Halisi YOTE YA MATIBABU.
Nenda ukaulizie kwa Mganga Mkuu
na Pia WIZARA YA AFYA Ili Watanzania popote walipo Wajue ni Kiasi Gani Kinahitajika kuokoa MAISHA YA KIJANA MWENZETU, MTOTO WETU, MJUKUU WETU.
Kama ni Milioni Ishirini useme KABISA Tsh /= 20,000,000 na Pia Utoe Details zote za Matumizi ya PESA hizo
kama Ni Milioni Thelasini na tatu mia Tano utuambie Kabisa Tsh/=33,500,000.
Kisha zoezi hilo Likianza la Ukusanyaji utoe ripoti kila siku kwamba umekusanya Kiasi Gani.
Na kila hatua Mpaka kwenye malipo pamoja na SAHIHI ZA MPOKEAJI ZIONEKANE na TAREHE PIA
TAFADHALI SANA FANYA HIVYO
KWA SABABU KUNA WATANZANIA WENGI SANA NA WASIO WATANZANIA WANATAKA KUSAIDIA KIJANA HUYU ILA WANASITA KWANI HAWAJUI GHALAMA ZA MATIBABU
AHSANTE
Inaatakiwa shiling ngapi, ili tupate picha kwenye viwango vya kuchangia.
ReplyDeleteMIMI NAITWA DR FRANK GEORGE MADINDA NI MKUU WA IDARA YA UPASUAJI ARUSHA LUTHERAN MEDICAL CENTRE AU KAMA INABYOJULIKANA NA WENGI SELIANI YA MJINI ILIYOKO ARUSHA
ReplyDeleteMLETENI HUYO MAMA NA MTOTO WAKE HUKU TUTAMSAIDIA KUMFANYIA OPERESHENI YA KUMTENGENEZEA NJIA YA KAWAIDA YA KUTOLEA CHOO.
NAMBA ZANGU NI HIZI 0788417112
NIPIGIENI TUONGEE TUNAWEZA KUSAIDIA BILA SHIDA
ASANTENI
DR MADINDA
Pole sana kwa Mtoto, Inasikitisha sana kuona serikali inashindwa chukua Jukumu dogo kama hili while watu tunalipa makodi mpaka basi. kulitakiwa kuwa na system ya kusaidia watu kama hawa jamani. Tatizo likingine ni uhalisia wa issue ilivyo na alie ileta hapa. Mimi naomba wewe ulioleta jambo hili hapa uende CCBRT au Huko Muhimbili, Upate gharama zote ikiwemo ya kulazwa hapo na chakula na wakupatie Invoice pamoja na account number ya hiyo hospital sisi wachangiaji tuingize huko hela. Dogo afanyiwe matibabu haraka. Sisi tunaochanga tutakuwa tunakutiumia kwa email zile deposit slip ili kama kuna chenji wakupatie umpe dogo.Au Ankali na Blogu yako chukeni jukumu la kukusanya michango na kutoa taarifa za michango na hali ya Dogo.
ReplyDeleteWengi tunataka kuchangia ila tunaomba huyo aliyeandika awe anaweka update, amefikia wapi. Tunaogopa tusije tukaingizwa mkenge na mitandao hii. Au aweke orodha ya watu waliochanga hapa, ili tusaidie haraka haraka jamani. Najua tunatoa kama sadaka lakini vile vile tumeguswa tunataka tuone pesa inatumika kwa kile ilichokusudiwa. Asante.
ReplyDeleteMpelekeni kwa Dr. Madinda kama mmekubali hivyo sisi tutachangia tunakokuelewa LUTHERAN MEDICAL CENTRE. Haya mambo ya kuchangia moja kwa moja kwa mtu nimeshalizwa sana...
ReplyDeleteHONGERA SANA DR. MADINDA KWA KUJITOLEA. NAOMBA MOLA AKUBARIKI NA AWACHOMOE GIZANI MADAKTARI WETU BINGWA ILI WALETE FARAJA HOSPITALINI KOTE TANZANIA
ReplyDeleteKitu kimoja nimekisoma hapa na naomba mkiache, sababu ni kukatishana tamaa.
ReplyDeleteHivi bila huyu mtoa taarifa kujitolea kuleta habari hii kwa Michuzi, mngefahamu vipi kwamba kuna msaada unahitajika?
Ahsante Dokta Madinda kujitolea, lakini nyie mnaotaka kila siku iendayo kwa Mungu mpewe ripoti, na kuanza kukosa imani kwa mchangishaji, wala sio watoaji.