Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Ndg Michuzi naandika ujumbe huu kwa uchungu mkubwa sana.Naomba ujumbe wangu uufikishe kwa viongozi wanaosimamia swala la viumbe wetu Mungu aliotujalia.Kinachoniuma roho ni jinsi vyombo vya usalama vinavyoonyesha mapungufu na madhaifu ya kuweza kuingizwa kwenye vitabu vya maajabu ya dunia.Hakuna nchi duniani inaweza kushindwa kukabiliana na na uhalifu na mbaya zaidi uhalifu huo ukifanywa na watu wa kuja.(wageni).tuliopo ugenini tunajua.swala hapa limekuwa kupambana na majangiri kwa ajili ya pembe tu ila wakati wachina wanakamatwa inaelekea kwa hisia zangu serikali yangu inawezekana imeruhusu hadi uuzwaji wa bidhaa za baharini.ikumbukwe kuwa hizo zote ni nyara zetu.Kama tunauza madini,ardhi,kila kitu kwa wageni kuna haja gani ya kuruhusu hizo biashara za ajabu ajabu? ziacheni wajukuu zetu nao wakija waone dunia ilivyoumbwa na mwenyeziMungu.Nilikuwa naongea na baadhi ya watu wa mataifa mbali mbali wanawafahamu sana wachina ni majanga mwisho wataanza hata kununua mafuvu ya watu.Jamani wanasiasa fanyezi kazi zenu kwa weledi mkubwa.wakati wa mangungo ulishapita.katika kusoma sheria za hapa uingereza nimegundua kuwa kadri mageuzi yanavyotokea kwenye jamii ndo na demand ya mabadiriko ya sheria inavyokuwa.sasa sheria lazima zibadilike kukabiliana na wimbi la uhalifu.kama hao wachina wanonekana kutoheshimu mali zetu na uafrika wetu werudi kwao si wenyewe tu wanaoweza kusaidia maendeleo yetu.peleka salamu zangu hadi bungeni kuwa safisha safisha ya wachina kwa mambo tuayodhania kuwa ni matakataka kwa kipiondi hiki lawama za kizazi kijacho zitawaangukia na hiyo dhambi itakitafuna kizazi hiki cha sasa.Na ikumbukwe kuwa matatizo yote yanaletwa na nyie mnaosimamia nchi yetu.haiwezekani mwekezaji anapanda ndege hadi tanzania kuja kulima bustani za nyanya,kufanya umachinga nk ujue tu kuna biashara nyingine nyingi zisizo halali wanazifanya chini kwa chini.Ndg mashaka alishawaambia wachina hawana jipya la kukomboa uchumi wa afrika miaka kama minne iliyopita na matokeo yake mnayaona.

    ReplyDelete
  2. Zamani pembe za ndovu tulikua tunazitumia kama ala ya muziki kwa kupuliza au mbiu ya mgambo kuitana kwa minajiri ya kukutana au hata mazishi,hali hii ya kutofahamu thamani ya pembe za ndovu inaendelea mpaka sasa kwa kuwaruhusu wageni wafanye watakavyo, hizi pilika za viongozi kujitutumua ni basi tu wafanyeje.

    ReplyDelete
  3. Michuzi, hii bonge la elimu! Je, waliotengeneza wanaweza waitafsiri kwa kiswahili na ruhusa iombwe hili tangazo lirushwe kwenye television zote Tanzania?

    Binafsi nachukua jukumu la kuweka link kwenye ukurasa wangu Facebook na naomba Mungu watu wabadilishane.

    ReplyDelete
  4. Ushauri Wangu ni huu kwa kuwa tembo wanateketezwa na majangiri kwa nini serikali isichukue jukumu au operation ya kuwakata tembo meno kama wavyofanya Botswana na Africa itasaidia vifo vya wanyama hao. Ahsanteeni

    ReplyDelete
  5. Kama tutaendele na Utamaduni mbovu na uliopitwa na wakati wa Kufumbiana macho na Kusadiana saidiana TUTAJIKUTA TANZANIA ILIYOKUWA NA IDADI YA MALAKI YA TEMBO KABLA YA UHURU (TEMBO ZAIDI YA 200,000) INABAKIWA NA TEMBO WAWILI (2) AMA MMOJA (1) AMA TUKALETEWA MBEGU YA TEMBO KUTOKA SCOTLAN-UINGEREZA KAMA TULIVYOLETEWA MBEGU YA FARU MWAKA JUZI 2012 KUTOKA UK!

    Ahhhh, sasa basi mzaha mzaha hutumbua usaha,,,hadi lini tutaendelea kukingiana vifua OHHH HUYU JAMANI INGAWA ANATUHUMIWA UJANGILI MWACHENI NI MWENZETU, OHHH HUYU TUMEKAA NAYE VIZURI TUMASAIDIE.

    HIVI JAMANI NCHI GANI DUNIANI INASAIDIA WAHAULIFU?

    ReplyDelete
  6. Kuwanusuru Tembo, Maliasili na wanyama Pori Majangili (Watakao patikana na uthibitisho kamili sio kuhisiwa aa kutuhumiwa) Wahukumiwe Adhabu ya Kifo ama Vifungo vya Maisha!!!

    ReplyDelete
  7. Is a Matter of logic and critical thinking!

    Hivi jamani Maharama na Majangili wanaua Tembo na kujinufaisha binafsi kwa mapato (wao na familia zao),,,Wakati Tembo, Maliasili na Wanyama Pori ndio Vivutio kwa Watalii vinavyoingiza Mapato (MABILIONI YA DOLA KWA MWAKA) kwa faida ya nchi kupata fedha za kuendeshea Serikali.

    SASA JE TUWASAIDIE MAJANGILI NA KUIKWAMISHA NCHI NA WANANCHI?

    AMA TUWAWAJIBISHE MAHARAMAIA NA MAJANGILI ILI KUNUSURU HATMA, MUSTAKABALI WA WANANCHI NA MASLAHI YA NCHI?

    JE, TUNATAKA DUNIA ITUELEWEJE?

    ReplyDelete
  8. Ningependa kuweka mchango wangu kuhusiana na swala hili muhimu km ifuatavyo
    -uwepo wa Wachina nchini si tatizo, na wako all over the world.vilex2 uwepo wa Wachina majangiri, si wao wakulaumiwa kwani hawa ni opportunists km watu wengine.Tatizo hapa lipo kwetu wenyewe, kwa kuifanya rushwa kama mfumo halali wa maisha na, kwa watanzania kukosa uzalendo.ikufahamike kuwa wachina hawa hawatoki kwao na kuingia kwenye mbuga zetu na kuua wanyama hawa bila kupata local support.na ukiangalia hapa ushiriki wa locals unakuwa facilitated through corruption.
    Lakusikitisha zaidi ni pale unapoona hata viongozi wa serikali wanasikitika,lalamika.wakati wako katika nafasi ya act.wamezungukwa na kila resource
    ie, nguvu za dola kumaliza tatizo hili.lkn zaidi agenda hii inafanywa kuwa kama mradi wa kisiasa zaidi.kinachotakiwa ni action sio takwimu, mikakati, makongamano, tume ..

    ReplyDelete
  9. Kwakweli sisi wafrica sijui tuna matatizo gani? yaani hata hatujielewi kabisa, hawa wanyama, mnyama kama tembo ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wote kwanza ni fahari yetu sisi, wafrica tumejaliwa, na hata ukiwaona wanapendeza na wanawakirisha bara hili, lakini tumekuwa na ujinga, ujinga wa kuto kujielewa, kila sehemu, kuanzia ngazi zote tumefeli, Hata kujiongoza wenyewe tunashidwa ni ujinga ujinga tu

    ReplyDelete
  10. Mnatakiwa kuandika kwa kifupi hayo maoni yenu jamani

    ReplyDelete
  11. Just like blood Diamonds, Except here the victim is the pride of our Nations, Elephants.

    ReplyDelete
  12. Hii kazi ya ujangili inafadhiliwa na viongozi wenywe. Kama ingekuwa watu wa kawaida wanaofanya ujagili hii shida ingeisha siku nyingi.

    Tulimwambia Kagasheki kuwa anapigana vita na watu asiowajua. kumbe mwishowe aliligundua hilo.

    Viondozi ndo wanataka kumaliza nchi

    ReplyDelete
  13. Hii inauma sana,

    Huu ni ubinafsi wa hali ya juu zaidi ambao binadamu tumefikia...!

    Kwa sensa inavyoonyesha Tembo wamepungua kwa nusu ya idadi kwa miaka chini ya mitano...!

    Huyu anayeua, hajui kuwa wakiisha wote na biashara yake itakufa...?!

    Jamani, huu ni umasikini wa kufikiri kama kesho itakuwaje, tunajua ni waafrika wanaowinda, ila biashara sio zao, sasa tukiua wote, tutaanza kuuza na meno ya binadamu, kama biashara mpya...!!!

    Inatisha, sijui mjukuu wangu ataishi dunia ya ukatili kiasi gani...??!!!

    INATISHA....!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...