MWANDISHI wa BBC kutoka nchini Kenya, Anne Waithera amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya saratani ya ubongo kwa takriban miaka miwili.
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.
Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia.Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV.
Ann aliyekuwa na umri wa miaka 39 anaelezwa na waandishi wenzake kuwa alikuwa mtu mzuri na hodari wa kazi.
Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema : "Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.''
Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann.
Poleni wafiwa
ReplyDelete