Mwenge wa Jumuiya ya Madola (Queens Baton Relay) leo umetembelea
Hospitali ya Taifa Muhimbili jumapili ukiongozwa na Mheshimiwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Dianna Melrose pamoja na mshindi wa mbio za kilomita 1500 za jumuiya ya madola Bw. Filbert Bayi.

Mwenge huu umetembelea Hospitalini hapa kwa nia kubwa ya
Kukutana na watoto wanaougua saratani mbalimbali ili kuwapa
matumaini ya kuishi na kwamba jamii inawanathamini. Watoto hawa
wamepata fursa ya kuushika mwenge huu na kupiga picha kama
kumbukumbu muhimu katika maisha yao fuatulia katika picha jinsi
watoto walivyofurahia mwenge huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela akipokea mwenge kutoka kwa kiongozi  wa michezo ya Olimpiki kutoka Kenya Bw. Kipchoge Keino
 Dkt. Njelekela akimkabidhi mwenge mtoto anayeugua ugonjwa wa saratani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...