Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali ameagiza kumalizwa kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire, Pori la Akiba la Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa muda wa takribani miaka kumi hadi sasa. Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hizo kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni kuleta migogoro isiyo ya lazima.

Mhe. Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara zilizokutana kwa ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo.

Aliongeza kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa kuishirikisha jamii kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kusimamia na kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote na kwa kuzingatia haki za binadamu.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara na Dodoma wakati wa kikao maalum cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Elaston Mbwilo akisitiza jambo wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
Sehemu wa wajumbe waliokutana katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Kutoka kulia: Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa na KatibuTawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Waheshimiwa Wabunge Zabein Mhita na Moza Abeid kutoka Dodoma wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na wanahabari mara baada ya kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kazana Mjomba, uwaziri kamili unanukia :)

    ReplyDelete
  2. piga kazi baba uukwae uwaziri kamili, fitna kwa kwenda mbele!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...