Mkurugenzi wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata mwongozo wa Umoja wa Mataifa.
Mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboje akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema juhudi zinahitajika katika kuwahamasisha Watanzania kumiliki viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
HII NI MIKAKATI TU, KAMA KUANZA MBONA TULIANZA MIAKA YA 60 AMA WENZETU WA MIKAKATI MMESAHAU? MNGESEMA KUVIFUFUA VILIVYOKUFA LABDA INGEELEWEKA, LAKINI PIA BILA KUJUA KIINI CHA KILICHOSABABISHA VIFO HIVYO ITAKUWA KAMA KINDA LA ATCL AMBALO KILA LIKITAKA KUTOTOKA KUTOKA KWENYE YAI LINASHINDWA! HAYA LETENI MIKAKATI YENU NASI TUNASUBIRI NA TUTASUBIRI NA KUSUBIRI.
ReplyDelete