Na
Mwandishi Maalum
Baraza
Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,
limeambiwa, kuna taarifa za uhakika na zisizo na shaka
kuwa kundi la waasi la M23
limeanza kujiunda na kujipanga upya.
Hayo
yameelezwa leo na Bw.
Martin Kobler (pichani), Mwakilishi wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
na Mkuu wa Misheni ya Kulinda Amani
katika DRC, ( MONUSCO).
Alikuwa akiwasilisha
mbele ya Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa, taarifa ya Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa kuhusu Misheni ya Kulinda Amani
ya Umoja wa Mataifa katika DRC (
MONUSCO).
“Tunazo taarifa za uhakika kabisa kwamba kundi
hili la M23 baada ya kusambaratishwa vibaya mwezi Novemba mwaka jana, sasa
limeanza kujiunda na kujipanga upya” akasema Bw. Kobler
Na
kuongeza, “ Ninapenda kutumia nafasi hii, kuitaka Serikali ya DRC kuanza
kutekeleza makubaliano ya Nairobi. Na
kwa nchi za Uganda na Rwanda kutoruhusu ardhi yao kutumiwa na kundi la M23 iwe
ni kujipanga upya au kwa mafunzo ya aina
yoyote ”.
Mbali
ya Mkuu wa MONUSCO kutoa taarifa yake
kwa Baraza hilo, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu katika
eneo la Maziwa Makuu, Bi. Mary Robinson naye aliwasilisha taarifa yake.
Mkuu
huyo wa Misheni ya MONUSCO alieleza
bayana kwamba makundi ya waasi
katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo bado ni tishio kubwa
katika mchakato mzima wa utafutaji wa Amani ya kudumu katika DRC na hususani
katika eneo la Mashariki ya nchi hiyo.
“Uwepo
wa Brigedi Maalum ( FIB) na matumizi ya ndege zisizoendeshwa na binadamu ( UAVs), makundi yote ya waasi
yanajua wazi kwamba, sasa tuna nia na uwezo wa
kutumia nguvu kubwa wakati
wowote”. Akasisitiza Mkuu huyo wa
MONUSCO.
Katika taarifa yake kwa Baraza Kuu la Usalama, Bw. Kobler , alielezea
kwa kina hali ya usalama ilivyo
nchini DRC na kazi kubwa inayofanywa
na MONUSCO katika kuyakabili makundi ya
waasi na vilevile kutoa ulinzi kwa raia.
Bw. Kobler alibainisha zaidi kwa kusema kuwa,“
Katika wiki zijazo, tutakuwa tumekamilisha mapitio
ya mkao wa kijeshi katika eneo lote
la Mashariki ya Kongo. Baada ya kukamilisha kazi hiyo tutakuwa na urahisi wa kwenda mahali popote na wakati wowote tunapohitajika, kukabiliana na tishio la
aina yoyote na kutoa ulinzi kwa raia “
Naye Bi. Mary Robinson, Mjumbe Maalum wa Katibu
Mkuu katika eneo la Maziwa Makuu, akizungumza kwa njia ya video
tele-conferencing kutokea Kishansa DRC, ameliambia Baraza Kuu la Usalama, kwamba wakati umefika sasa kwa nchi
zile zilizotia saini Mpango Mpana wa Umoja wa Mataifa kuhusu Siasa, Usalama na Maendeleo katika DRC na Maziwa
Makuu kuanza kutekeleza maamuzi magumu.
Akasema juhudi za
kutafuta Amani na usalama katika
DRC zipo katika kipindi muhimu hivi sasa na kutoa wito kwa viongozi
waliosaini mpango huo kuanza kutelekeza ahadi zao ili hatimaye Amani iweze
kupatikana.
Bi.
Robinson ambaye kesho ( Jumanne) atahudhuria mkutano wa Wakuu
wa Nchi za Maziwa Makuu ( ICGLR)utakaofanyika nchini Rwanda alieleza pia kwamba,
mazingira ya utulivu yaliyokuwapo
baada ya kusambaratishwa kundi la M23
yamepotea na kwamba eneo hilo sasa lipo
katika kipindi cha kurejea kwa
machafuko.
Akasema
utulivu huo umetoweka hasa baada
ya kutokea kwa mashambulizi yaliyofanywa
na kundi la waasi la Alliend Democratic Forces ( ADF) katika
eneo la Mashariki ya DRC.
Aidha
kuendelea kwa hali ya machafuko
katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuibuka kwa mapigano katika Sudan ya Kusini,pia kumechangia kuwepo
mdororo huo wa kiusalama mashariki ya DRC.
Na
kwa sababu hiyo anasema, utekelezaji wa
mpango mpana wa kisiasa bado unabaki kuwa
suluhu pekee ya upatikanaji
wa Amani ya kudumu, usalama, ushirikiano
na maendeleo katika eneo la Maziwa
Makuu.
ReplyDeletenini chanzo haswaa kinacho pelekea sisi waafrika kumalizana wenyewe kwa wenyewe ni mpaka lini tutachoka na hivi vita vya kijinga??
inakua aibu sana kila mahali unaposema umetoka africa wanadhani umetoka kwenye sehemu ya vita
Safari hii hayo madege yasiyo na marubani yaruhusiwe kuingia hadi nchi jirani za Uganda na Rwanda ikibidi wanakosemekana wanafanyia mafunzo na kambi zao za kijeshi ili mchawi ajulikane ni nani!
ReplyDeleteSi nimesikia kati za nchi wafadhili wa M23 zimeomba 'po' ziliposikia kuna midege iso na rubani....
ReplyDeleteAfu UN wanan'gata na kupuliza...hapa hakuna mazungumzo ni kutandika tu...mazungumzo gani wakati hawa watu nia yao ni kuvura amani tu ili waibe dhahabu...
How many7 times wamepewa chance ya kukaa mezani?
Mchawi si mwingine ni PK na YKM hawa ndo matatizo yote ya East Africa kwa ujumla UN hawa watu mnawabeba sana na mnawajua.Kitawageukia ninyi subiri.
ReplyDelete