Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharib,Mh. Juma Ngasongwa amenusurika kifo katika ajali iliyo tokea jana jioni maeneo ya Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani.

Ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Rav 4 mali ya Mh. Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam wakati akielekea Mkoani Morogoro,ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Shirika la Umeme (Tanesco) lenye Nambari za Usajili SU 37199 na kupelekea kutokea kwa ajali hiyo.

Mh. Ngasongwa alikimbizwa Hospitali ya Tumbi,Kibaha na kuanza kupatiwa matibabu mara moja na baadae alihashiwa Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili katika taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.
Pichani anaonekana Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mh. Mwantumu Mahiza akimjulia hali Mh. Ngasongwa alipokuwa kwenye Hospitali ya Tumbi Kibaha alipo fikishwa kwa ajili ya huduma ya kwanza.katikati ni Dkt. Loti Kiwelu wa Hospitali hiyo.
 Mh. Ngasongwa akisaidiwa na muuguzi wa Hospitali ya Tumbi.
Hii ndio gari iliyosababisha ajali hiyo.
Hivi ndivyo ionekanavyo Gari aliyokuwa akiendesha Mh. Ngasongwa.Picha na Chriss Mfinanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kwa maelezo ya habari hapa inaonekana lori(dereva) wa tanesco ana makosa hivyo wajiandae kumlipa fidia mheshimiwa Ngasongwa.

    ReplyDelete
  2. kazi ya kumlipa mh Ngasongwa ni ya insurance si ya Tanesco- kama gari ina bima

    ReplyDelete
  3. Pole sana mzee Ngasongwa.Na kwanini tunaandika kwamba hili ndilo lori lilisosababisha ajali hiyo na siyo hiyo RAV4?Kazi ya TRAFIKI hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...