Home
Unlabelled
NEWZ ALERT:MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM YAHIRISHA KUTOA UAMUZI WA MAOMBI YA ZITO KABWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
a) Wajerumani walipokuwa wakiingia Tanganyika kabla ya Waingereza, walitengeneza urafiki mkubwa sana kati yao na Watanganyika kiasi kwamba Watanganyika wakawaamini na wakawakaribisha. Watanganyika wakaamini kuwa pengine walikuwa tayari wamepata watu ambao wangeweza kusaidiana nao kuyatatua matatizo yao, lakini ikawa kinyume pale Wajerumani walipodhihirisha unafki wa urafiki waliouanzisha na hao Watanganyika. Ninaweza kumfananisha Zitto na hao Wajerumani. Zitto alitumia moyo wake wote na nguvu zake zote kutuaminisha Watanzania kuwa alikuwa na uchungu na Nchi yetu hasa pale alipoamua kupigana na ufisadi na uadui mwingine kati 2005 na 2010. Kumbe hiyo yoye ilikuwa ni mbinu ya yeye mwenyewe kuwa kama Wajerumani.
ReplyDeleteb) Nikumungalia kutokea upande wa viongozi wa jadi wa Tanganyika wa miaka ile, namfananisha Zitto na Mangungo wa Msovero Usagara Kilosa aliyeishi na kuongoza watu wake miaka iliyopita na hatimaye kuwauza kwa wakoloni. Zitto alikuwa na dhamira ya kuiuza CHADEMA na Wanachadema kwa Wadharimu na Wazandiki wa Taifa letu, CCM akisahau kuwa kati ya 2005 na 2010 baada ya yeye kusimamishwa kuingia bungeni alizunguka Nchi nzima na kusema mengi sana dhidi ya CCM. Nakumbuka moja ya hotuba zake aliyozotoa katika ziara hiyo pale Tukuyu, Wilayani Rungwe, Zitto alisema,"CCM wanataka kutuuza kama Mangungo wa Msovero Usagara alivyo tuuza kwa Wajerumani, wanahistoria watakuwa wanaungana nani katika hili". Akaongezea kwa kusema, "Tuungane pamoja kuwapinga CCM". Sasa sijui alituhamasisha tuungane naye kivipi kama yeye mwenyewe kwa akili zake mwenyewe (to the best of his knowledge) kaamua kuuza Mustabali wa Taifa zima kwa wadharimu na Wazandiki, CCM?
Nimeishiwa maneno ya kusema. Natamani wanasiasa wetu waone hiyo comment hapo juu.
DeleteJamani, magomvi ya Chadema CCM inaingizwa vipi? Yakiwashinda mnatafuta mchawi!!!
ReplyDeleteNguvu zote hizo mnzotumia kumsakama Zitto, kwani mmepungukiwa kiasi gani hata hamuoni yanayotendeka CHADEMA??!!. Poor you souls muombe mola awaondolee mapepo mkubali kukosoana kwa hoja, kila mmoja akivumilia na kutafakari hoja aliyotoa mwenzake na kujirekebisha. Ukomavu huo wa Demokrasia ndio utakaowajengea heshima kwa jamii ya Tanganyika Kama mnataka legitimacy ya kutuongoza.
ReplyDeletekama kawasaliti wanachadema poleni ila sisi watanzania bado tunamuamini kutetea maslahi ya watanzania. Kama Mbunge kafanya na bado anaendelea kufanya mengi.
ReplyDeletemtoa comment wa kwanza bila shaka we ni mtu kati ya wale wanaemchukia tu zitto bila sababu ya msingi,..unatuleteaje story ya wajerumani haina mahusiano kabisa na magomvi ya akina zitto na wenziwe?kwa nini usijikite ktk hoja walizoziandika?huo mfano wako haufanani hata kidogo na uhalisia wa mambo,..nakupa pole sana kama we ni miongoni mwa watu wanaoamini chadema ndicho ukombozi wa watz,..kwa dalili zote chadema ni genge la wahuni tu wanaotumia mgongo wa watanzania kama wewe,..na historia ya german/wakoloni na haya ya akina zitto haifanani kabisa usitudanganye!
ReplyDeleteHii ni aibu kwa watu wanaotaka madaraka kwa kutaka kuwazunguka wenzao. Zitto kweli kama alikuwa na njama za kuwasaliti wana chadema ni halali ang'olewe. Mimi naamini kabisa chadema bila Zitto kabwe inawezekana! Watapatikana wanasiasa wengine ambao ni mahiri kuliko hata yeye. M4C endeleeni na mapambano njia ni nyeupe peee.
ReplyDeleteWatoa comments wa 2 hadi 6, nasikitika kusema kuwa, "Inawezekana huwa mnaangalia mwisho wa jambo pekee na sio mwanzo wala katikati ya jambo lenyewe". Kwa kuwasaidia naweza sema, "Jaribuni kuujua mwenendo wa Zitto Kabwe ndani ya Chama tangu mwaka 2008 to-date itawasaidieni japo kupata uelewa kidogo tu". Hata shule ina taratibu na kanuni ambazo kila mmoja lazima azifuate na kuziheshimu na yeyote anayekwenda kinyume anawajibishwa bila kujali umaarufu wake binfsi au ule unaomzunguka. This principle applies to CHADEMA, kama Zitto kashindwa na amezisaliti taratibu na katiba ya chama, hana budi kuwajibishwa ili kujenga dhana nzima ya UWAJIBIKAJI ambayo CHADEMA inahubiri. "CHADEMA should walk the talk" si kama ilivyo kwa chama/vyama vingine vya siasa vinavyofyata mikia yao na kushindwa kuwawajibisha wakosaji wao sababu ya sura zao na ubabe wao. Mtu mwenye kujua kesho hawezi kukumbatia wadharimu wa leo.
ReplyDelete