Kwanza kabisa naanza kumpongeza mdogo wangu Flaviana kwa kazi nzuri anayofanya ya kusaidia jamii hasa kupitia mfuko wake wa Flaviana Matata Foundation wa kusaidia watoto ili waweze kuipenda shule zaidi.
Sasa nilikuwa naomba tena aongeze na jingine hasa nilikuwa na mkubunsha kuikumbuka jamii ya kabira ya Wanyambo wanaopatakana mkoa wa kagera wilaya ya karagwe na Kyerwa kama sikosei ndilo kabila lako. kumekuwa na tabia kukatishwa masomo watoto wa kike hasa wanaosoma sekondari kwa kweli hilo ni tatizo la wilaya zetu.
Kwa sababu amesema tumuunge mkono naomba na hilo aliweke kwenye program yake ilii mfuko wake uweze kulifanyia kazi. watoto wa kike wamekuwa wakikatishwa masomo kwa kubebwa kwa lazima (yaani mtu anaoa kwa lazima ) naomba kupitia mfuko wako tulipige vita ni tabia ambayo imeishapitwa na wakati.
mdau
Elewa
Karagwe
Na tunabaki kila siku kuwa Tanzania hakuna ukabila, ilhali bado tunatizamana kwa asili yetu mtu anapofanya jambo lolote lile jema au baya kabila yake itaangaliwa na kutajwa tu!!!
ReplyDeleteKulikuwa na haja gani kutaja asili yake iiwa tu lengo lako ni kumuomba aangalie tatizo la watoto wa kitanzania wa sehemu fulani Tanzania kukatishwa masomo?
Ndugu yangu Mnyambo,
ReplyDeleteusilete ukabila hapa kwanini wewe usifanye kazi hiyo, mabadiliko ni wewe ni mimi ni sisi. Kila mtu akaianza kurudi kushughulika kwao na wasiokuwa na bahati ya walisonga mbele kimaisha itakuweje? ni vizuri kurudisha nyumbani lakini kumbuka sisi ni Watanzania hivyo ni kabila moja!!!!!!!!!!!
Tribalist. you got me when you said kabira badala ya kabila.
ReplyDeleteVinginevyo hongera sana Flavian.
Elewa,
ReplyDeleteSijui hata jina 'Elewa' ni lako kweli make haliendi na jinsi ulivyoleta tatizo..
Ulichoongea ni tatizo kweli, kosa ni kwamba badala ya kumwomba Flaviana kama mtanzania mwenzako unaomba msaada wake kwasababu ni kabila lako.
Vile vile, kwa tatizo kama hilo ningekushauri kuongea na afisa elimu wa Wilaya au ikishindikana nenda kwa mkuu wa Wilaya